Msanii wa Mongolia ya Ndani, China atumia mawe ya Mto Manjano kuyachora michoro mbalimbali

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 11, 2024
Msanii wa Mongolia ya Ndani, China atumia mawe ya Mto Manjano kuyachora michoro mbalimbali
Lu Ting (kushoto) akichora kwenye jiwe. (Picha na Wu Yana)

Mji wa Wuhai ni kituo ambacho Mto Manjano huingia katika Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, China, na msanii Lu Ting wa Wuhai amezaliwa na kukulia kando ya Mto huo Manjano, mto unaosifiwa kuwa “Mto Mama” nchini China.

“Maji ya Mto Manjano yanarutubisha ardhi ya kaskazini ya China,” amesema Lu, huku akikumbuka kuwa jambo lililofurahisha zaidi wakati alipokuwa akisoma shuleni, ni wakati mwalimu alipowaongoza wanafunzi wenzake kwenda kuokota mawe kwenye pwani ya Mto Manjano.

Mnamo mwaka 2016, baada ya karibu miaka 20 ya kufundisha, Lu Ting alianza rasmi kuchora kwenye mawe kwa kutumia ufundi wake wa uchoraji.

Lu amemfahamisha mwandishi wa habari kuwa: “Mwanzoni niliokota mawe saba, nikabuni hadithi na kuchora mfululizo wangu wa kwanza wa ‘Picha za Watoto wa Mto wa Bakara’.”

Mnamo 2018, Lu alifungua Studio ya Uchoraji wa kwenye Mawe ya Mto Manjano katika Kijiji cha Saihanwusu kando ya Mto Manjano. Amesema: “Nina ndoto ya kutumia mawe ya Mto Manjano kusimuliza simulizi za furaha katika kijiji hiki ambazo zinahusiana na mila na desturi za wenyeji.”

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha