Kundi la 45 la Jeshi la Majini la China lawasili Madagascar kuanza ziara ya kirafiki

(CRI Online) April 11, 2024
Kundi la 45 la Jeshi la Majini la China lawasili Madagascar kuanza ziara ya kirafiki
Kundi la 45 la Jeshi la Majini la China likiwasili katika Bandari ya Tuamasina, Madagascar kuanza ziara ya kirafiki, Aprili 10, 2024. Katika picha hii askari wa kundi hilo wanaonekana wakiwapungia mikono watu waliokuja kuwakaribisha. (Picha na Wang Yuanfang/Ilichapishwa na Xinhua)

Kundi la 45 la Jeshi la Majini la China limewasili katika bandari ya Tuamasina, Madagascar siku Jumatano kuanza ziara ya kirafiki ya siku tano.

Kwenye hafla ya kuwakaribisha, Madagascar iliandaa ngoma za Dragoni na Simba, na ngoma za kienyeji za nchini humo, na wawakilishi wa wanafunzi waliwavisha mataji ya maua makamanda wa jeshi hilo.

Wakati wa ziara hiyo, pande hizo mbili zitafanya shughuli mbalimbali zikiwemo za kutembelea kambi za jeshi na kufanya mashindano ya kirafiki ya michezo, pia wanajeshi wa majini wa China watatembelea shule za wanafunzi wenye asili ya China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha