China yafukua kaburi la kiwango cha juu zaidi la Dola ya Kale ya Chu kuwahi kuchimbuliwa hadi sasa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 17, 2024
China yafukua kaburi la kiwango cha juu zaidi la Dola ya Kale ya Chu kuwahi kuchimbuliwa hadi sasa
Wanaakiolojia wakifanya kazi kwenye kaburi la Wuwangdun lililogunduliwa Huainan, Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China, Aprili 6, 2024. (Idara ya Kitaifa Mabaki ya Kale ya Kitamaduni ya China/ Xinhua)

HEFEI - Kaburi la Wuwangdun lililofukuliwa katika Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China limethibitishwa kuwa kaburi kubwa na la ngazi ya juu zaidi ya Dola ya Chu ya China katika zama za kale iliyokuwepo katika kipindi cha zaidi ya miaka 2,200 iliyopita, Idara ya Kitaifa ya Mabaki ya Kale ya Kitamaduni ya China imesema Jumanne.

Idara hiyo imetangaza habari hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari katika Mji wa Huainan, na kuongeza kuwa kaburi hilo lililogunduliwa huko Huainan ndiyo lenye muundo wenye utatanishi zaidi wa aina yake.

Waakiolojia walijikita katika kufukuliwa kwa kaburi kuu la shimo la ardhini lililo wima, na kulithibitisha kuwa jengo kubwa lililo na eneo la kuzikia la mbao.

Watafiti wamefanya ulinzi wa eneo husika na utafiti mbalimbali wa kitaaluma za mabaki ya kale yaliyofukuliwa, wakiimarisha na kufukua vitu dhaifu kama vile mbao za chemba, mikeka ya mianzi na kitambaa kigumu.

Uchambuzi wa wakati mmoja ulihusu teknolojia ya kaboni-14, utambuzi wa spishi za miti, uchanganuzi wa aina za mbao, uchambuzi wa maandishi kwenye kaburi, na utafiti wa nyenzo na utengenezaji wa vitambaa vigumu na mavazi.

Idara hiyo pia imeahidi kuendelea na kazi ya kiakiolojia, uhifadhi wa mabaki ya kale ya kitamaduni na utafiti wa taaluma mbalimbali huko Wuwangdun, kwa lengo la kutoa mwanga juu ya mila na desturi za Dola ya Chu katika kipindi cha mwisho cha Madola ya Mapigano, ufundi wa Sanaa na mafanikio ya kitamaduni.

Kipindi cha Madola ya Mapigano cha China ya zama za kale kilianzia 475 B.K. hadi 221 B.K.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha