Kampuni za kimataifa zatafuta fursa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi ya China mkoani Hainan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 18, 2024
Kampuni za kimataifa zatafuta fursa katika Maonyesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi ya China mkoani Hainan
Watu wakitembea katika ukumbi wa Maonyesho ya nne ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi ya China huko Haikou, mji mkuu wa Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, Aprili 17, 2024. (Xinhua/Guo Cheng)

HAIKOU - Katika Maonyesho ya nne ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi ya China yanayoendelea Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China, mfanyabiashara kutoka Uturuki, Ramazan Tuzen apokea watu wengi kwenye banda lake.

Huu ni mara yake ya tatu mfululizo kushiriki katika maonyesho hayo ya Hainan, na ameleta bidhaa mbalimbali za Uturuki kwenye maonyesho ya mwaka huu. Bidhaa hizo ni pamoja na vipodozi, bidhaa za kauri za kazi za mikononi na nguo na vitambaa za nyumbani, ambazo baadhi yao zinaonyeshwa kwenye maonyesho hayo kwa mara ya kwanza.

"Bidhaa za kauri zinatengenezwa kwa mikono, na hizi ni vitu vya kitamaduni kutoka Uturuki. Zinakaribishwa sana hapa," Tuzen amesema, akiongeza kuwa karibu bidhaa zake zote zinapokelewa vizuri na watembeleaji wa banda lake.

Akiwa anafanya biashara hiyo kwa miaka 15 sasa, Tuzen anaona fursa kubwa katika soko la China, na anatarajia kupata fursa zaidi nchini China ili kupanua biashara yake.

"Tunataka kuwa na washirika na wasambazaji wa ndani ya China, na ndiyo sababu tuko hapa kwenye maonyesho," amesema, huku akiongeza kuwa Uturuki ni nchi ya kuvutia, na bidhaa zake zenye mambo ya kitamaduni zinafuatiliwa sana katika maonyesho hayo.

Ireland, wakati huo huo, ni nchi mgeni wa heshima katika maonyesho ya mwaka huu, ikiwa na kampuni na taasisi jumla ya 29 za Ireland zinazoshiriki katika maonyesho hayo. Kwenye banda la Ireland, vyakula vya kijani vilivyoidhinishwa vinavutia wateja -- huku watu wengi wakijitokeza kujaribu bidhaa hizo.

Conor O'Sullivan, Meneja wa Bodi ya Chakula ya Ireland nchini China, amesema kutokana na wateja wa China kuzingatia zaidi uendelevu wa mazingira katika matumizi yao ya kila siku ya chakula, Ireland inafaa kwa sababu imeanzisha mpango uliothibitishwa ya uendelevu kwa sekta yake ya chakula.

"Hii inafanya bidhaa za Ireland zitoshee kabisa mahitaji haya mapya ya bidhaa za kijani katika soko la China," O'Sullivan amesema.

Maonyesho hayo ambayo yameanza Aprili 13 na yatafikia tamati leo Aprili 18, ni maonyesho pekee ya ngazi ya kitaifa ya China yanayohusisha bidhaa za matumizi na pia ni maonyesho makubwa zaidi ya bidhaa za matumizi katika eneo zima la Asia-Pasifiki.

Yakiwa na kaulimbiu ya "Changia Fursa za Wazi, Jenga kwa pamoja Maisha Bora" maonyesho hayo yana kiwango kikubwa zaidi hadi sasa, yakivutia chapa zaidi ya 4,000 kutoka nchi na maeneo 71, yakichukua eneo la maonyesho la ndani lenye ukubwa wa mita za mraba 128,000. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha