Marekani yarejesha kwa China vitu 38 vya mabaki ya kale ya kitamaduni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 18, 2024
Marekani yarejesha kwa China vitu 38 vya mabaki ya kale ya kitamaduni
Naibu Waziri wa Utamaduni na Utalii wa China ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Kitaifa Mabaki ya kale ya kitamaduni ya China, Li Qun (wa pili kulia) na Matthew Bogdanos (wa pili kushoto), mkuu wa Kitengo cha Usafirishaji Haramu wa Vitu vya Mabaki ya Kale ya Kitamaduni katika Ofisi ya Idara ya Uendeshaji wa Mashtaka ya Eneo la Manhattan, wakitia saini nyaraka kwenye hafla ya makabidhiano ya vitu vya mabaki ya kale ya kitamaduni vya China yaliyorejeshwa katika Ubalozi Mdogo wa China huko New York, Marekani, tarehe 17 Aprili 2024. (Xinhua/Li Rui)

NEW YORK - Upande wa Marekani umerejesha vitu 38 vya mabaki ya kale ya kitamaduni vya China kwa upande wa China siku ya Jumatano ambapo kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Ubalozi Mdogo wa China mjini New York, Ofisi ya Idara ya Uendeshaji wa Mashtaka ya Eneo la Manhattan la New York, Marekani imekabidhi vitu hivyo vya mabaki ya kale ya kitamaduni kwa ujumbe wa Idara ya Kitaifa ya Mabaki ya Kale ya kitamaduni ya China.

China na Marekani zilitia saini makubaliano ya kumbukumbu ambayo yanalenga kuzuia uingizaji haramu wa mabaki ya kale ya kitamaduni ya China nchini Marekani Januari 2009. Muda wa kufanya kazi kwa makubaliano umeongezwa kwa mara ya tatu, kuanzia Januari 14 mwaka huu. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha