Mradi wa ustawi wa umma waonesha mfano wa urafiki wa China na Angola

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 18, 2024
Mradi wa ustawi wa umma waonesha mfano wa urafiki wa China na Angola
Wakazi wakitembea kwenye bustani ya "mji mpya" wa Kilamba katika kitongoji cha Luanda, Angola, Machi 7, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

Ukiwa unapatikana umbali wa kilomita 18 kusini mwa Luanda, mji mkuu wa Angola, "mji mpya" wa Kilamba unaonekana wazi kwenye upeo wa macho. Zaidi ya muongo mmoja baada ya kukamilika kwake, ujenzi wa mradi huo mkubwa wa ustawi wa umma, uliofanywa na kampuni za China, unajumuisha majengo 700 na nyumba zaidi ya 20,000 za makazi, ukitoa hali ya kisasa ya maisha kwa wakazi wake 120,000.

Mji huo wa Kilamba, ambao zamani ulijulikana kwa jina la Mradi wa Nyumba wa Kilamba Kiaxi, ulianzishwa na kampuni ya Ujenzi ya CITIC ya China. Ndani yake kuna majengo ya kutosha yakiwemo shule, kiwanda cha kushughulikia maji na vituo vya kupozea na kusambaza umeme, ili kuhakikisha wakaazi wanafurahia maisha mazuri.

Ukiwa umejengwa kutoka kwenye ardhi iliyokuwa duni, mji huo mpya ni ushuhuda wa ushirikiano unaokua kwa kasi kati ya nchi hizo mbili. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha