Mafuriko makubwa yaukumba Mkoa wa Guangdong, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 22, 2024
Mafuriko makubwa yaukumba Mkoa wa Guangdong, China
Picha iliyopigwa tarehe 21 Aprili 2024 ikionyesha eneo lililokumbwa na mafuriko katika Hanguang mjini Qingyuan, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. (Xinhua/Huang Guobao)

GUANGZHOU – Idara ya Uhifadhi wa Maji ya Mkoa wa Guangdong imesema kuwa, vituo 38 vya upimaji wa kiwango cha maji kwenye mito 24 katika Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China vimeripoti viwango vya maji vyenye kuvuka kiwango cha tahadhari hadi ilipokuwa imefika saa kumi jioni siku ya Jumapili.

Maeneo ya chini ya Mto Beijiang yalikuwa yakitazamiwa kukumbwa na mafuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Kamati ya kupunguza maafa ya mkoa huo imetangaza hatua ya mwitikio wa dharura ya Ngazi ya IV ili kukabiliana na mafuriko hayo yaliyoikumba miji ya Shaoguan na Qingyuan mkoani Guangdong. Juhudi za uokoaji pia zinaendelea.

Maofisa wa serikali ya huko wamesema, watu jumla ya 652 wamehamishwa na kupata makazi mapya ipasavyo katika Tarafa ya Longgui huko Shaoguan. Wafanyakazi zaidi ya 200 wa usafi wa mazingira wametumwa mara moja kuondoa matope na miti iliyoanguka mitaani, na kushughulikia njia za maji na mifereji ya maji.

Idara ya ufuatiliaji wa hali ya hewa ya Mkoa wa Guangdong imetabiri mvua kunyesha mara kwa mara hadi wiki ijayo katika mkoa huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha