Mji wa Roma, Italia waadhimisha miaka 2,777 tangu kuanzishwa kwake

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 22, 2024
Mji wa Roma, Italia waadhimisha miaka 2,777 tangu kuanzishwa kwake
Watu wakishiriki katika mashindano ya askari wa kale katika eneo la Circus Maximus huko Roma, Italia, Aprili 20, 2024. (Xinhua/Li Jing)

ROMA - Mji Mkuu wa Italia, Roma siku ya Jumapili umesherehekea miaka 2,777 tangu kuanzishwa kwake, ambapo siku hiyo ulilipuka kwa matamasha, maonyesho, sherehe na kanivali iliyohusisha watu zaidi ya 2,000 wakiandamana kwa kuigiza wanajeshi wa dola la kale la Warumi, maakida, maseneta, wapiganaji wa visu, miungu ya kale ya Warumi, makasisi, na watawala, wote wakiwa wamevalia mavazi kamili ya enzi ya Warumi.

"Ni njia ya kuheshimu historia ya mji wetu huku tukijifurahisha na kujionyesha kwa wageni na wanafunzi," Marco Contarini, mfanyakazi wa mkahawa mwenye umri wa miaka 29 ambaye ameshiriki kwenye kanivali hiyo akiwa amevalia kama askari kamanda wa enzi ya Warumi, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

Mji wa Roma ulianzishwa Aprili 21, 753 B.C na sherehe hiyo ambayo hufanyika kila mwaka tarehe hiyo, katika miaka ya hivi karibuni imekua maarufu kwa watalii

Sherehe hiyo ya Jumapili imefanyika huko Circus Maximus, uwanja wa zamani wa mbio wa enzi ya Warumi ambao uko katika eneo la chini kati ya Palatine na Aventine, vilima vyenye uhusiano wa kina na historia ya mji huo.

Preston Juan Loria, meneja wa miradi kutoka Florida, Marekani, mwenye umri wa miaka 49, amesema kuwa kukutana na sherehe hiyoni jambo la kufurahisha akiwa likizoni mjini humo.

"Hatukupanga kuja Roma kwa sherehe ya kuadhimisha siku ya kuanzishwa kwake lakini kuona haya yote ni njia nzuri ya kutumia sehemu ya siku moja, kuona mambo yote," Loria ameliambia Xinhua. "Nimependa sana kuona tofauti, mavazi ya kale katika mji wa kisasa."

Ingawa chanzo cha sherehe hiyo ya Jumapili kinaanzia karne nyingi zilizopita, shughuli zake zimekumbana na watalii kwani utalii nchini Italia unaimarika kutoka kwenye athari za janga la virusi vya Korona.

Hakuna makadirio rasmi ya idadi ya watu walioshiriki katika shughuli hizo za Jumapili, vyombo vya habari vimeripoti kuwa mji huo ulikuwa umeweka polisi wa ziada kwa usalama na udhibiti wa usafari na matumizi ya barabara. Oda za hoteli zilikuwa juu kuliko kawaida mwishoni mwa wiki, habari zilizoripotiwa na vyombo vya habari zimesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha