Mji wa Luoyang, China wafuata na kujikita katika utamaduni unaohusiana na maua ya peony

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 23, 2024
Mji wa Luoyang, China wafuata na kujikita katika utamaduni unaohusiana na maua ya peony
Mfanyakazi akichora feni ya mkononi yenye kauli mbiu ya maua peony kwenye bustani ya mimea huko Luoyang, Mkoa wa Henan, Katikati ya China, Aprili 17, 2024. (Xinhua/Li Jianan)

Ukiwa ni mji mkuu wa kifalme katika enzi 13 za China ya kale, Mji wa Luoyang ulio katika Mkoa wa Henan, Katikati ya China unatambulika kwa kuwa na maua bora zaidi ya peony nchini humo. Katika miaka ya hivi karibuni, mji huo umekuwa ukifuata na kujikita kikamilifu katika utamaduni unaohusiana na maua hayo, ukihimiza shughuli za utengenezaji wa vyombo vya kauri, uchoraji wa michoro yenye maudhui ya maua ya peony, na shughuli nyingine nyingi zinazohusiana na maua hayo. Maendeleo haya huwezesha watalii kufurahia maua na mandhari ya mji huo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha