Kikosi cha Majini cha PLA chafanya shughuli za wazi kwa umma kwa kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwake

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 23, 2024
Kikosi cha Majini cha PLA chafanya shughuli za wazi kwa umma kwa kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwake
Watoto wakijifunza lugha ya bendera kwenye gati namba 3 katika Bandari ya Qingdao, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, Aprili 21, 2024. (Xinhua/Li Ziheng)

Kikosi cha Wanajeshi wa Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) kimefanya shughuli za wazi kwa umma katika miji mingi ya pwani ikiwa ni pamoja na Mji wa Qingdao, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China kuanzia siku ya Jumatatu, Aprili 23 ili kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwake.

Kuanzia Aprili 20 hadi 24, watu wa Qingdao wataweza kutembelea manowari za kuangamiza makombora za Guiyang, Shijiazhuang na Kaifeng, manowari ya makombora ya Handan, manowari ya Kekexilihu ya utoaji wa mahitaji kwa manowari nyingine , na manowari ya uokoaji ya Hongzehu kwenye gati namba 3 na gati ya Kituo cha Kimataifa cha Usafiri wa majini cha Qingdao.

Manowari nyingi kati ya hizo zilishiriki katika operesheni kubwa kama vile operesheni ya kufanya doria katika Ghuba ya Aden, kutembelea bandari za ng'ambo na kufanya mazoezi ya pamoja.

Licha ya mji huo Qingdao, kikosi hicho cha majini cha China kimesema kitaandaa siku ya shughuli za wazi kwa umma kwenye kambi zake katika miji mingine, ikiwemo Dalian, Yantai, Ningbo, Wuhan, Xiamen, Guangzhou, Haikou na Sanya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha