China na Cambodia kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya kiwango cha juu, sifa bora na kigezo cha juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 23, 2024
China na Cambodia kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya kiwango cha juu, sifa bora na kigezo cha juu
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Naibu Waziri Mkuu wa Cambodia Sun Chanthol wakishiriki kwenye hafla ya kufungua mauzo ya nazi ya Cambodia nchini China baada ya kuongoza kwa pamoja mkutano wa saba wa Kamati ya Uratibu kati ya Serikali za China na Cambodia mjini Phnom Penh, Cambodia, Aprili 22, 2024. (Picha na Sovannara/Xinhua)

PHNOM PENH - China na Cambodia zimeahidi siku ya Jumatatu kufanya juhudi zaidi za kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya China na Cambodia yenye mustakabali wa pamoja iliyo ya kiwango cha juu, ya sifa bora na kwa kigezo cha juu.

Pande hizo mbili zimefikia makubaliano mapana kuhusu mwelekeo wa juhudi zao katika hatua inayofuata ya ujenzi wa jumuiya hiyo ya nchi hizo mbili na kupitia kikamilifu kazi ya utekelezaji wa mpango kazi wa kujenga jumuiya hiyo kwenye mkutano wa saba wa Kamati ya Uratibu kati ya Serikali za China na Cambodia uliofanyika Phnom Penh, mji mkuu wa Cambodia.

Mkutano huo uliongozwa kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Naibu Waziri Mkuu wa Cambodia Sun Chanthol.

Kwenye mkutano huo, Wang amesisitiza kuwa China na Cambodia zinafurahia urafiki wa chuma unaoendana na maslahi ya watu wa nchi hizo mbili na mwelekeo wa maendeleo ya zama hizi, zikijivunia hamasa kubwa na matarajio mapana.

Wang amesisitiza kuwa, chini ya mwongozo wa kimkakati wa viongozi wa nchi hizo mbili, ujenzi wa jumuiya ya China na Cambodia yenye mustakabali wa pamoja umekuwa kielelezo cha kuunda aina mpya ya uhusiano kati ya nchi na nchi.

Ametoa wito wa kufanyika juhudi za pamoja katika kuendeleza urafiki wa jadi, kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa, kuimarisha ushirikiano wa pande zote, kuzidisha mfumokazi wa ushirikiano wa "Almasi ya Hexagon", na kuendeleza miradi ya kujenga Ukanda wa Maendeleo ya Viwanda na Ukanda wa Samaki na Mpunga.

Pande hizo mbili zimekubaliana mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuharakisha uoanishaji wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja la China na Mkakati wa Pentagonal wa Cambodia, uundaji wa mpango wa ushirikiano wa Ukanda wa Maendeleo ya Viwanda, kazi ya usanifu wa reli ya China na Cambodia, na utekelezaji wa programu za uvunaji wa mapema wa Ukanda wa Samaki na Mpunga.

Pia zitasukuma mbele utekelezaji wa kiwango cha juu wa Mkataba wa Biashara Huria kati ya China na Cambodia, kuunga mkono mauzo ya mazao ya kilimo ya Cambodia yenye sifa bora nchini China, na kuhimiza kampuni zaidi za China kuwekeza nchini Cambodia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha