Makumbusho ya Liangzhu: Eneo la kuufahamu ustaarabu mzuri wa China wa miaka 5,000 iliyopita

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 26, 2024
Makumbusho ya Liangzhu: Eneo la kuufahamu ustaarabu mzuri wa China wa miaka 5,000 iliyopita
Mwelezaji wa kujitolea wa Jumba la Makumbusho ya Ustaarabu wa Liangzhu Emma Chen (kushoto) akimwelezea mwanahabari wa People’s Daily Online (kulia). (Picha/Yuan Meng)

Timu ya wanahabari ya People’s Daily Online ya “kutazama China” hivi karibuni imetembelea Liangzhu kujionea ustaarabu wa zama za kale wa China. Jumba la Makumbusho ya Ustaarabu wa Liangzhu lipo ndani ya Bustani ya Meilizhou, Mtaa wa Liangzhu, eneo la Yuhang, Mji wa Hangzhou katika Mkoa wa Zhejiang, China. Jumba hilo ni makumbusho ya eneo la kiakiolojia inayokusanya, kutafiti, kuonesha na kueneza mambo ya ustaarabu wa Liangzhu.

Magofu ya Liangzhu ni sehemu muhimu sana ambayo inathibitisha historia ya miaka 5,000 ya ustaarabu wa China. Kwenye jumba hilo la makumbusho, kuna kumbi tatu za “nchi ya kubarikiwa katikati ya maji”, “Nchi Takatifu Iliyostaarabika” na “Jade, roho ya nchi”, ambazo zinaonesha kwa kina, kiuhalisia na kwa pande zote mafanikio ya kiakiolojia na thamani ya urithi ya magofu ya Liangzhu na ustaarabu wa Liangzhu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha