Meli zarudi kwenye bandari kwa msimu wa kusitisha uvuvi unaokaribia nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 30, 2024
Meli zarudi kwenye bandari kwa msimu wa kusitisha uvuvi unaokaribia nchini China
Picha iliyopigwa tarehe 29, Aprili ikionesha meli za uvuvi zinazotia nanga kwenye bandari ya uvuvi ya Shenjiamen ya eneo la Putuo la Mji wa Zhoushan wa Mkoa wa Zhejiang, China. (Picha/Yao Feng)

Kuanzia saa 6 mchana (kwa saa za Beijing), ya tarehe Mosi mwezi Mei, msimu wa kusitisha uvuvi baharini utaanza katika maeneo ya bahari ya China, yakiwemo bahari ya Bohai, bahari ya Huanghai, bahari ya Mashariki na sehemu ya bahari ya Kusini iliyopo kaskazini ya latitudo 12°N. Hivi sasa meli za uvuvi za maeneo hayo zinarudi kwa mfululizo kwenye bandari, zikifanya maandalizi kabla ya wakati ili kukaribisha msimu wa kusitisha uvuvi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha