Picha:Kuingia shule ya lugha za Kihungaria na Kichina na kuhisi mvuto wa mawasiliano ya utamaduni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 10, 2024
Picha:Kuingia shule ya lugha za Kihungaria na Kichina na kuhisi mvuto wa mawasiliano ya utamaduni
Mei 8 kwa saa za huko, wanafunzi wa shule ya lugha za Kihungaria na Kichina wakicheza dansi ya China iliyopendwa na watoto wengi. (Mpiga picha: Su Yingxiang/People's Daily Online)

Shule ya lugha za Kihungaria na Kichina iliyoko Budapest ndiyo shule ya kipekee ya umma katika Ulaya ya Kati na ya Mashariki ambayo inatumia lugha ya Kichina na lugha ya Kihungaria. Shule hiyo ilianzishwa mwezi Septemba, Mwaka 2004. Katika miaka 20 iliyopita, shule hiyo imewaandaa wanafunzi wengi wanaofahamu na kupenda utamaduni wa China, na imejenga daraja la urafiki kati ya China na Hungary. Mwaka 2023, Rais Xi Jinping alijibu barua kutoka wanafunzi wa shule hiyo, akiwahimiza vijana wa Hungary kuijua zaidi China na kuwa mabalozi wa kurithi na kuendeleza mambo ya urafiki kati ya China na Hungary. Hebu tufuate waandishi wa habari wa People's Daily Online kuingia shule hiyo na kuangalia "mabalozi hao wa baadaye wa mambo ya urafiki kati ya China na Hungary".

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha