Kiwanda cha Mimea: Uwanja mpya wa Uzalishaji wa Kilimo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 13, 2024
Kiwanda cha Mimea: Uwanja mpya wa Uzalishaji wa Kilimo
Mikono ya roboti ikifanya uzalishaji kiotomatiki katika kiwanda cha mimea huko Quanzhou, Mkoa wa Fujia,China Mei 8, 2024. (Picha/Xinhua)

Mfumo wa uzalishaji wa mimea wenye ufanisi wa hali ya juu, ambapo mazingira ya ukuaji wa mimea yanawezesha kufikia udhibiti kamilifu kwa kutumia akili mnemba, umetumika katika kiwanda cha mimea cha kiotomatiki cha kikazi kipya katika Mkoa wa Fujian, China.

Katika kiwanda hicho cha mimea, kilimo cha mboga hakihitaji jua na udongo. Kwa sasa mazao ya kila siku ya mboga yanaweza kufikia tani 1.5, na usambazaji endelevu wa mazao umefikiwa katika maeneo ya karibu kama vile miji ya Fuzhou, Xiamen na Quanzhou.

Mbunifu na mwendeshaji wa mfumo huo, kampuni ya Sanan Sino-Science iliyoanzishwa mwaka 2015, ni ubia wa Taasisi ya Mimea chini ya Akademia ya Sayansi ya China na kampuni ya Sanan ya teknolojia ya mwanga wa jua yenye makao makuu yake mjini Xiamen.

Teknolojia ya kampuni hiyo ya LED na ya biolojia ya nuru zimefika katika nchi na maeneo 33 zikiwemo Marekani, Japan na Singapore.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha