

Lugha Nyingine
Misri yafanya jaribio la kwanza la teksi zinazotumia umeme katika Mji Mkuu Mpya wa Utawala nchini humo (5)
![]() |
Teksi zinazotumia umeme zikionekana kwenye shughuli ya jaribio katika Mji Mkuu Mpya wa Utawala, Misri, Mei 15, 2024. (Xinhua/Ahmed Gomaa) |
CAIRO - Misri ime jaribio la kwanza la matumizi ya teksi siku ya Jumatano katika Mji Mkuu Mpya wa Utawala (NAC) wa nchi hiyo, kwa lengo la kutoa chaguo la rafiki wa mazingira na usafiri wa kisasa.
Awamu hiyo ya kwanza imehusisha magari 10 yanayotumia umeme yakitumika katika mji huo mpya, ambao kwa sasa ni makao makuu ya wizara nyingi na taasisi za serikali ya Misri.
Magari yanayomilikiwa na Wizara ya Uchukuzi ya Misri, yanajumuisha magari 85 yaliyotengenezwa na kampuni ya MG4 ya China na magari 60 ya kampuni ya Chevrolet Bolt. Yatasimamiwa na kampuni ya nchini Misri.
"Magari haya 10 ya kwanza yanayotumia umeme yanaashiria hatua ya kwanza," George Michael, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Suluhu ya Usafiri unaotumia Nishati Safi ya Caesar, ambayo ni mwendeshaji wa mradi huo, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua, akionyesha uingizaji wa haraka wa magari yaliyobakia katika huduma hiyo na kuwa uwezekano wa kutoa huduma nje ya mipaka ya NAC.
"Magari haya mapya yanayotumia umeme ni salama sana... yana mifumo ya kufuatilia usalama ya ndani na nje, na vifaa vya GPS ili kuhakikisha usalama wa abiria wakati wa safari," Michael amesema.
Ameongeza kuwa, licha ya usalama, mradi huo unaendana na msukumo wa Misri wa kuwa na suluhisho la kisasa na endelevu za uchukuzi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma