

Lugha Nyingine
Maisha mapya ya wanandoa wa Hunan Changsha wenye matatizo ya kusikia (5)
![]() |
Zhan Jingwen (Kati) akihudhuria darasa katika kituo cha kuimarisha na kujenga upya afya ya usikivu huko Changsha, Mkoa wa Hunan, katikati ya China, Mei 16, 2024. (Xinhua/Chen Zhenhai) |
Ingawa Zhang Yongsheng na mkewe Zhan Jingwen ni wanandoa wenye matatizo ya kusikia waliweza kumfanya binti yao, ambaye pia ana tatizo hili , kuweza kusikia akiwa na umri wa miaka miwili.
Kwa kuendesha duka la vitafunio kwenye soko la usiku na shukrani kwa msaada kutoka kwa jamaa na marafiki zao, wanandoa hao wameweza kumudu upandikizaji wa mrija wa sikio (cochlear) kwenye sikio la kushoto na kifaa cha kuwezesha usikivu kwa sikio la kulia la binti yao huyo. "Ni ghali sana kuwa na matibabu kama hayo kwangu na mke wangu, na tayari hata hivyo tumezoea dunia ya kimya. Tunachotaka ni kuhakikisha binti yetu anakuwa na uwezo wa kusikia."
Mapema mwaka huu, wakati simulizi ya familia hiyo ilipoenezwa na mwanablogu, kwa kushangaza walipokea salamu na misaada mingi ya wema na faraja kutoka kwa watu wasiowafahamu.
Shukrani kwa vifaa vya kuwezesha usikivu vilivyotolewa kwao mwezi Januari, Zhang Yongsheng aliweza kumsikia binti yake akiita "baba" kwa mara ya kwanza wakati wa siku yake ya kuzaliwa ya miaka 32. Mwezi Machi, kwa usaidizi kutoka kwa kampuni ya mirija ya sikio, cochlear, familia hiyo ilifanyiwa operesheni ya upandikizaji wa mirija ya sauti kwenye masikio, cochlear mjini Shanghai. Baada ya takriban mwezi mmoja wa kupata nafuu, wakati vipandikizi vyao hivyo vya usikivu vilipowashwa na kuunganishwa, watatu hao wa familia hiyo waliweza kusikia sauti za kila mmoja kwa mara ya kwanza.
Tangu mwezi Mei, wamekuwa chini ya mafunzo ya bure ya kusikia na kuzungumza yanayotolewa na kituo cha kuimarisha na kujenga upya afya ya mwili huko Changsha. Baba na mama pia hujifunza kuzungumza kutoka mwanzo chini ya "mwongozo" wa binti yao. Zhang anatumai kwamba siku moja ataweza kusaidia watu wengine wenye matatizo kusikia sauti za ajabu za dunia hii.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma