Rais wa Iran pamoja na Waziri wake wa Mambo ya Nje wafariki katika ajali ya helikopta (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 20, 2024
Rais wa Iran pamoja na Waziri wake wa Mambo ya Nje wafariki katika ajali ya helikopta
Picha hii iliyopigwa Mei 19, 2024 ikionyesha skrini inayoonyesha video iliyorushwa na kituo cha televisheni ya taifa ya Iran kuhusu kazi ya utafutaji na uokoaji baada ya helikopta kutua kwa kishindo katika Jimbo la Azarbaijan Mashariki, Iran. (Xinhua/Shadati)

TEHRAN –TEHRAN - Rais Ebrahim Raisi wa Iran na Waziri wake wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian wamefariki katika ajali ya helikopta, vyombo vya habari mbalimbali vimeripoti siku ya Jumatatu ambapo, shirika la habari la Iran, Mehr limethibitisha kutokea kwa vifo hivyo, likiripoti kwamba "abiria wote wa helikopta iliyokuwa imembeba rais wa Iran na waziri wake wa mambo ya nje wameuawa kishujaa."

Awali Makamu wa Rais wa Iran anayehusika na masuala ya Utendaji Mohsen Mansouri alikiambia kituo cha televisheni ya taifa ya Iran, IRIB kwamba kutua kwa kishindo kwa helikopta hiyo kulikuwa kumetokea katika Jimbo la kaskazini-magharibi la Azarbaijan Mashariki siku ya Jumapili.

Mansouri alisema kuwa eneo hilo la kutua lilikuwa limepunguzwa katika zoezi la utafutaji na uokoaji hadi ukubwa wa karibu kilomita 2, lakini eneo husika la tukio lilikuwa bado halijajulikana na kazi ya utafutaji na uokoaji ilikuwa bado ikiendelea polepole katika eneo ambalo ilikuwa ni vigumu kufikiwa lililoathiriwa na hali mbaya ya hewa.

Alisema tukio hilo lilitokea mapema Jumapili katika Kaunti ya Varzaqan, umbali wa takriban kilomita 670 kutoka mji mkuu Tehran na kwamba mawasiliano yalikuwa yameanzishwa na mmoja wa abiria na wahudumu waliokuwa ndani ya helikopta hiyo ingawa hata hivyo hakutaja utambulisho wa watu hao.

Raisi alikuwa akisafiri kwenye msafara wa helikopta tatu wakati ambapo helikopta hiyo iliyokuwa imembeba ilipopoteza mawasiliano na nyingine mbili dakika takriban 30 baada ya kupaa.

Helikopta nyingine mbili mara moja zilianza utafutaji katika eneo hilo kwa takriban dakika 20, lakini baadaye zililazimika kutua kwa dharura kutokana na ukungu mzito na hali nyingine ya hewa, NBC assassin Mansouri amebainisha.

Akizungumza kwenye mkutano na familia za wanajeshi wa IRGC wa Iran mjini Tehran, Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei amewaambia wananchi wa Iran wasiwe na wasiwasi kwani hakutakuwa na mvurugiko wowote katika masuala ya nchi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha