

Lugha Nyingine
Vijana wa makabila madogo washuhudia ustawi wa kijiji katika Mkoa wa Guangxi, China
Mwaka 2007, Wu Xinren, kijana wa kabila la Wamiao mwenye umri wa miaka 28, alimaliza maisha yake ya miaka kumi ya kufanya kazi mjini na kurudi, na mke wake wa miaka 22, He Yuqing, katika kijiji cha nyumbani kwake cha Wuying pamoja na mke wake mwenye umri wa miaka 22, He Yuqing, kijiji ambacho ni chenye watu wachache wa Kabila la Wamiao kilichoko kwenye milima mirefu inayovuka mpaka kati ya Mkoa unaojiendesha wa Kabla la Wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China na Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China.
Tangu wakati huo, Wu na mkewe wamekuwa wakijaribu kuanzisha huko biashara kuanzia kilimo, uchukuzi hadi kuendesha duka la mboga mboga na kutoa huduma ya malazi kwa wageni ikiwa ni pamoja na kuuza bidhaa za kienyeji.
Maisha yao ya kitamaduni pia yamestawi huku biashara yao ikiwaletea hali bora ya maisha. Kwa miaka mingi, wameshuhudia maendeleo ya kijiji chao kustawishwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma