Maonyesho ya kimataifa ya mambo ya kitamaduni yafunguliwa katika Mji wa Shenzhen, Kusini mwa China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 24, 2024
Maonyesho ya kimataifa ya mambo ya kitamaduni yafunguliwa katika Mji wa Shenzhen, Kusini mwa China
Watu wakitazama onyesho la opera ya Yueju kwenye Maonyesho ya 20 ya Kimataifa ya Mambo ya Kitamaduni ya China (Shenzhen) (ICIF) yaliyofanika katika Kituo cha Maonyesho na Mikutano cha Kimataifa cha Shenzhen, mjini Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Mei 23, 2024. (Xinhua/Liang Xu)

SHENZHEN - Maonyesho ya 20 ya Kimataifa ya Mambo ya Kitamaduni ya China (Shenzhen) (ICIF) yamefunguliwa Alhamisi katika mji wa Shenzhen, kusini mwa China ambapo kwa mara ya kwanza, maonyesho hayo ya siku tano yameanzisha maonyesho ya kimataifa ya biashara ya utamaduni, yakiwa na eneo la maonyesho linalochukua eneo la ukubwa wa mita za mraba 20,000.

Ukumbi mkuu wa maonyesho hayo ni katika Kituo cha Maonyesho na Mikutano cha Kimataifa cha Shenzhen. Yanajumuisha mabanda manane yanayojikita katika mambo kuhusu uvumbuzi wa kitamaduni wa Eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao, ufungamanishaji wa utamaduni na utalii, michezo na michezo ya kielekitroniki, na Guochao, ambayo pia inajulikana kama mitindo ya China au "China chic" .

Maonyesho maalum ya "China ya Utamaduni na Uvumbuzi" yameanzishwa kwenye maonyesho hayo ili kuonyesha mafanikio mapya yaliyopatikana katika kuendeleza uhamishaji wa uvumbuzi na maendeleo ya kibunifu ya utamaduni mzuri wa jadi wa China.

Kwa mujibu wa waandaaji, maonyesho hayo, yanayofanyika nje ya mtandao na mtandaoni kwa wakati mmoja, yamevutia mashirika zaidi ya 6,000 ya serikali, ya kitamaduni na kampuni, na vitu zaidi ya 120,000 vinavyoonyeshwa.

Waonyeshaji zaidi 300 kutoka nchi na kanda 60 wanashiriki katika maonyesho hayo.

Maonesho hayo yaliyoanzishwa mwaka 2004, yamekuwa shughuli ya kitamaduni inayoongozwa nchini China na jukwaa muhimu la kuhimiza utamaduni wa China kwenda duniani kote.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha