Hayati Rais wa Iran Raisi azikwa katika mji wa nyumbani kwake wa Mashhad (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 24, 2024
Hayati Rais wa Iran Raisi azikwa katika mji wa nyumbani kwake wa Mashhad
Watu wakimwomboleza hayati Rais wa Iran Ebrahim Raisi kwenye huko Mashhad, Kaskazini Mashariki mwa Iran, Mei 23, 2024. (Xinhua)

TEHRAN - Hayati Rais wa Iran Ebrahim Raisi, ambaye alipoteza maisha katika ajali ya helikopta hivi karibuni, amezikwa siku ya Alhamisi katika madhabahu takatifu ya Imam Reza katika mji wa nyumbani kwao, Kaskazini Mashariki mwa mji wa Mashhad ambapo mwili wake pamoja na ile ya maofisa wawili wa timu aliyokuwa ameambatana nayo, iliwasili na kuzikwa katika hafla ya mazishi iliyofanyika mapema siku hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran, IRNA, miili hiyo iliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mashhad Alhamisi alasiri kutoka Birjand, mji mkuu wa jimbo la mashariki la Khorasan Kusini huku katika uwanja huo wa ndege maofisa kadhaa wa Iran, wakiwemo mawaziri na makamanda wakuu wa kijeshi, kama vile Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Wanajeshi Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Esmaeil Qaani walikuwepo kusubiria.

Meya wa Mashhad, Mohammad-Reza Qalandar Sharif ameliambia IRNA kwamba watu takriban milioni 3 kutoka Mashhad na miji mingine wameshiriki kwenye mazishi, na kusababisha gari lililokuwa limebeba miili ya Raisi na wenzake kusimama kwa muda mara kadhaa likiwa njiani kupita mitaa iliyojaa watu wengi kuelekea kwenye hekalu takatifu.

Miili ya watu wengine wawili, Gavana wa Azarbaijan Mashariki Malek Rahmati na mkuu wa timu ya usalama ya rais Mehdi Mousavi, itazikwa katika majimbo ya Azarbaijan Mashariki na Tehran, kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari vya Iran.

Raisi na msafara wake walikuwa wakielekea Jimbo la Azarbaijan Mashariki wakati helikopta iliyokuwa imewabeba ilipoanguka katika eneo la milima siku ya Jumapili.

Ndani ya helikopta hiyo pia walikuwemo Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian na Mohammad Ali Ale-Hashem, mwakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Iran, Azarbaijan Mashariki.

Amir-Abdollahian alizikwa siku ya Alhamisi katika hafla iliyofanyika kusini mwa mji mkuu wa Iran, Tehran, kwa mujibu wa IRNA.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha