Reli ndefu zaidi kati ya miji katika eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao ya China yazinduliwa (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 27, 2024
Reli ndefu zaidi kati ya miji katika eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao ya China yazinduliwa
Treni ya kwanza ya reli ya kati ya miji kutoka Foshan hadi Dongguan ikifika kwenye Stesheni ya Reli ya Machong huko Dongguan, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Mei 26, 2024. (Xinhua/Liu Dawei)

GUANGZHOU - Sehemu mbili za reli katika eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao ya China zimezinduliwa siku ya Jumapili, ikionesha kufunguliwa kwa njia ndefu zaidi ya reli ya kati ya miji katika eneo hilo. Zhang Qiao, mhandisi mkuu wa Kampuni ya Kendesha Reli ya Kati ya Miji ya Guangdong amesema kuwa reli hiyo italeta urahisi kwa wenyeji wa huko, ambao wataweza kuipanda kama vile kupanda treni za sabwei.

Njia hiyo, inayounganisha miji ya Huizhou, Dongguan, Guangzhou, Foshan, na Zhaoqing kutoka mashariki hadi magharibi, ina urefu wa kilomita 258 na stesheni 39 kwa jumla za treni za kawaida, lakini treni za mwendo kasi husimama kwenye stesheni 14 kati ya hizo. Kasi ya juu ya treni hiyo ni kilomita 200 kwa saa, na wastani wa muda kati ya treni moja na nyingine inayofuata ni dakika 26.

Abiria wanaweza kununua tiketi kwa kutumia programu rasmi ya 12306 ya kuweka oda ya tiketi ya reli mtandaoni au kutumia kadi zao za usafiri wa umma.

Katika miaka ya hivi karibuni, China imeimarisha mafungamano ya mawasiliano kwenye Eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao. Shirika la Uendeshaji Treni za Sabwei la Guangzhou limekadiria kuwa ifikapo mwaka 2035, ukubwa wa uendeshaji wa usafiri wa reli katika Eneo la Ghuba Kuu hiyo utafikia kilomita 7,500, ikifikia miji yote juu ya ngazi ya wilaya na asilimia 80 ya miji yenye idadi ya watu iliyopangwa ya zaidi ya watu 50,000.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha