

Lugha Nyingine
Israel yathibitisha "tukio la kufyatuliana risasi" kwenye mpaka wa Misri (3)
![]() |
Wanajeshi wa Israel wakionekana karibu na mpaka na Ukanda wa Gaza, Kusini mwa Israel, Mei 27, 2024. (Picha na Gil Cohen Magen/Xinhua) |
JERUSALEM - Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limethibitisha kutokea kwa "tukio la kufyatuliana risasi" kwenye "mpaka wa Misri," baada ya vyombo vya habari vya Israel kuripoti kuzuka kwa kufyatuliana risasi kati ya wanajeshi wa Israel na Misri kwenye kivuko cha Rafah siku ya Jumatatu.
"Saa chache zilizopita kulikuwa na tukio la kufyatuliana risasi kwenye mpaka wa Misri, tukio hilo linachunguzwa, na tunafanya mazungumzo na upande wa Misri," IDF imesema.
Gazeti la Jerusalem Post la Israel limeripoti kuwa mwanajeshi wa Misri ameuawa katika tukio hilo, huku kituo cha Channel 14 cha Israel kikisema hakuna kifo kilichotokea.
Gazeti la kila siku la Israel la Maariv limenukuu vyanzo vya habari ndani ya IDF vikisema kuwa wanajeshi wa Misri waliwafyatulia risasi kwanza wanajeshi wa Israel, ambao nao walijibu kwa kuwafyatulia risasi.
Hata hivyo, Al Araby, chombo cha habari chenye makao yake makuu nchini Qatar, kimenukuu chanzo cha Misri kikisema kuwa IDF ilianzisha mapigano.
Kituo cha Channel 13 cha Israel kiliripoti mapema siku hiyo ya Jumatatu kwamba "tukio lisilo la kawaida" lilikuwa limetokea kati ya wanajeshi wa Israeli na wale wa Misri kwenye kivuko cha Rafah.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma