

Lugha Nyingine
Ligi Kuu ya Kijiji ya China yakita mizizi kwenye viwanja vya mpira wa miguu nchini Benin (6)
![]() |
Picha iliyopigwa Mei 25, 2024, ikionyesha hafla ya kutoa tuzo kwa washindi baada ya fainali ya mashindano ya kwanza ya “Ligi Kuu ya Kijiji” ya Afrika huko Parakou, Benin. (Xinhua/Li Yahui) |
PARAKOU, Benin - Benin inapokaribia msimu wake wa mvua, manyunyu ya vipindi na hali ya hewa ya joto hata haviwezi kupunguza shauku ya wanakijiji waliokusanyika kutazama fainali ya mchezo wa kwanza wa "Ligi Kuu ya Kijiji" ya Benin
Siku ya Jumamosi, timu za kandanda kutoka vijiji viwili vya Parakou, mji wa katikati ya Benin, zilichuana katika fainali ya mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Kijiji. Mechi hiyo ilifanyika kwenye uwanja wa mpira ulio karibu na kituo cha Wachina cha kusaidia uzalishaji wa pamba huko Benin, katika Kijiji cha Belle Cite. Ushindani mkali na burudani ya kuvutia ya soka viliibua shangwe kutoka kwa watazamaji wenye shauku.
Hatimaye, timu kutoka Kijiji cha Barrage ilitwaa ubingwa. Huku kukiwa na sauti ya muziki, timu tatu bora zilitunukiwa medali, vikombe na zawadi kwenye jukwaa.
Mohamed Gbeha, shabiki wa timu iliyofika fainali ya Park 7 ambaye pia ni mkulima wa pamba, ameelezea uungaji mkono wake kwa timu yake na shukrani kwa mradi wa China kwa kuandaa ligi hiyo ya soka. Amesema mara nyingi amekuwa akiomba ushauri kutoka kwa wataalamu wa China kuhusu mbinu za kukuza pamba.
Katika muongo mmoja uliopita, mradi wa teknolojia ya pamba unaotekelezwa kwa msaada wa China umekuwa ukifanya kazi huko Parakou, eneo kubwa linalozalisha pamba nchini Benin.
Wataalamu hao wa China wamekuwa wakifanya majaribio, kueneza mbinu za upandaji pamba, kutoa kielelezo kuhusu ufundi wa mashine za kilimo na kutoa mafunzo kwa wafundi wenyeji wa kilimo.
Msaada huo wa kitaalamu wa muda mrefu umekuza uhusiano imara na wanakijiji wa eneo hilo. Timu ya mradi huo ikiongozwa na Shou Xiaoyong ilipogundua kwamba uwanja wa mpira wa miguu ambao wanakijiji wamekuwa wakiutumia kucheza mpira ulikuwa umepokonywa, waliamua kujenga uwanja mpya kwa kutumia mashine za kilimo na vifaa vilivyobadilishwa matumizi.
Katika majira ya joto ya Mwaka 2023, video za baadhi ya mechi za soka za Ligi Kuu ya Kijiji ya China katika Wilaya ya Rongjiang, Eneo linalojiendesha la Makabila ya Wamiao na Wadong la Qiandongnan katika Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China, zilisambaa kwa kasi na kuvutia watalii duniani kote.
Ikiwa imehamasishwa na hili, Ligi Kuu ya Kijiji huko Parakou inajumuisha maonyesho ya kitamaduni wakati wa mapumziko, ambayo ni pamoja na sanaa ya Wushi ya China na ngoma ya jadi ya Benin.
"Wenyeji wanapenda soka na nilitaka kuleta mtindo huu hapa na kuanzisha ligi kama hiyo," Shou amesema.
Machi 2024, kwa uungaji mkono wa Shirikisho la wakulima wenyeji, wataalam wa China walipanga Ligi Kuu ya kwanza ya Vijiji nchini Benin.
Mashindano hayo yalishirikisha timu 12, wakiwemo wanakijiji kutoka vijiji sita vya wenyeji na timu kutoka Chuo Kikuu cha Parakou, wakiwa ni pamoja na wakulima wa pamba, madereva wa matrekta, maseremala na wanafunzi.
Kwa mujibu wa mkuu wa timu hiyo ya ufundi ya China, kuchanganya msaada wa kiufundi wa kilimo na Michezo ya soka ya Ligi Kuu ya Vijiji siyo tu kwamba kunakuza teknolojia ya juu ya kilimo bali pia kunaimarisha mawasiliano ya watu kati ya China na Benin. "Mtindo huu unaongeza uaminifu na heshima kwa misaada ya China miongoni mwa watu wa Benin," amehitimisha.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma