Uwekezaji wa China wasaidia Uganda kusukuma mbele maendeleo ya viwanda na mambo ya kisasa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 29, 2024
Uwekezaji wa China wasaidia Uganda kusukuma mbele maendeleo ya viwanda na mambo ya kisasa
David Bahati, Waziri wa Nchi wa Uganda anayeshughulikia biashara, viwanda na vyama vya ushirika, akizungumza kwenye mahojiano mjini Kampala, Uganda, Aprili 6, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

MBALE, Uganda – Wakati mapambazuko yanapowadia, Hellen Mugala, mwenye umri wa miaka 27, pamoja na mamia ya wafanyakazi wenzake wakielekea kazini kwenye Eneo Maalum la Viwanda la China na Uganda la Mbale, lililoko katika wilaya ya mashariki ya Uganda ya Mbale. "Eneo hili maalum la viwanda limesaidia watu wengi wenyeji. Nimepata ujuzi na kujipatia riziki kutoka kwa kampuni za China," Mugala amesema.

Kwa mujibu wa mamlaka ya eneo hilo, vijana takriban 5,000 wanapitia lango la eneo hilo kila siku, wakielekea kwenye viwanda mbalimbali. Eneo hilo maalum la viwanda ambalo moja ya maeneo makubwa zaidi ya viwanda nchini humo, lina kampuni zaidi ya 40 zinazotengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo simu janja, televisheni, nguo na chuma.

Wafanyabiashara wadogo na vijiji vya jirani pia vinapata faida kutokana na kuwepo kwa wafanyakazi wengi. Charles Nyeko, mkazi wa kijiji cha Doko, amesema jamii yake imebadilika sana kwani idadi ya watu imeongezeka kutoka 2,000 hadi takriban 4,000, wengi wao wakiwa ni wafanyakazi katika eneo hilo la viwanda. Tangu kufungua duka dogo kijijini hapo, maisha ya Nyeko "yameboreshwa zaidi."

Hadi kufikia mwisho wa Mwaka 2022, kwa upande wa uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) pekee, kampuni za China zilikuwa zimewekeza dola za Kimarekani zaidi ya milioni 692 nchini Uganda, kwa mujibu wa ubalozi wa China nchini humo. Mwaka 2023, FDI za China nchini Uganda zilifikia dola za Kimarekani milioni 55.7. Uwekezaji huu, hasa unaotimizwa kupitia Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja la China, umetoa makumi ya maelfu ya fursa za kazi kwa wenyeji.

Maafisa wa Serikali ya Uganda wamesema uwekezaji huo wa kasi unachochea maendeleo ya viwanda ya nchi hiyo na lengo kuu la ujenzi wa mambo ya kisasa.

David Bahati, Waziri wa Nchi wa Uganda anayeshughulikia Biashara, Viwanda na Ushirika, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kuwa China, mshirika muhimu wa ushirikiano wa Uganda, imekuwa ikitoa mtaji pamoja na kubadilishana ujuzi na teknolojia ili kuendeleza miundombinu ya nishati na usafiri, ambayo ni nguvu muhimu za kuhimiza maendeleo ya viwanda.

“Maendeleo ya Eneo Maalum la Viwanda la China na Uganda la Mbale yanafanya maajabu, tumeshuhudia FDI zinazoingia kupitia eneo hilo la viwanda, zikitusaidia katika mbadala wa bidhaa kutoka nje ya nchi. Vitu vingi ambavyo tulikuwa tukiagiza kutoka nje ya nchi kama televisheni na nguo vyote vinatengenezwa katika eneo hilo," Bahati amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha