Mto Yuehe katika Mji wa Jiaxing, Zhejiang, China: Kuonja Jiangnan wakati wa Sikukuu ya jadi ya Duanwu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 30, 2024
Mto Yuehe katika Mji wa Jiaxing, Zhejiang, China: Kuonja Jiangnan wakati wa Sikukuu ya jadi ya Duanwu
Watalii wakitembelea Mtaa wa Yuehe katika Mji wa Jiaxing, Mkoa wa Zhejiang, China, Mei 26. (Picha na Ge Taiyi, People's Daily Online)

Siku ya tano ya mwezi wa tano kwa kalenda ya kilimo ya China ni Sikukuu ya jadi ya Duanwu ya China, pia inajulikana ni siku ya mashindano ya mashua ya Dragoni, wakati sikukuu hiyo inapokaribia, watalii wanaotembea na kusimama kwenye barabara za Mtaa wa Kale wa Yuehe huko Jiaxing wakiwa nyuma ya mandhari ya kuta nyeupe na vigae vyeusi huunda picha nzuri ya mandhari ya Jiangnan ambayo ni sehemu ya kusini mwa Mto Changjiang.

Mtaa wa Kihistoria wa Jiaxing Yuehe ni mtaa wa kale mkubwa zaidi na wenye mpangilio kamilifu zaidi wa kihistoria katika Mji wa Jiaxing, eneo la mtaa huo lina mita za mraba 90,000, ambapo majengo 29 ya kihistoria yamehifadhiwa vizuri mtaani. Katika miaka ya hivi karibuni, kwa kupitia njia ya kuhifadhi majengo ya kale, mguso wa haiba ya kale umeonekana wazi katika mji huo ulioko kusini mwa Mto Changjiang huku kukiwa na ustawi wa kisasa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha