

Lugha Nyingine
Bustani ya Wanyama ya Kitaifa ya Washington nchini Marekani kupokea panda wawili kutoka China ifikapo mwisho wa mwaka (2)
![]() |
Bidhaa zenye muundo wa panda zikionekana kwenye Bustani ya Kitaifa ya Wanyama ya Smithsonian huko Washington, D.C., Marekani, Mei 29, 2024. (Xinhua/Liu Jie) |
WASHINGTON – Bustani ya Kitaifa ya Wanyama huko Washington, D.C., Marekani imetangaza siku ya Jumatano kuwa itapokea watoto wawili wa panda, mmoja dume na mwingine jike, kutoka China mwishoni mwa mwaka huu ambapo taarifa kwa vyombo vya habari ya Taasisi ya Kitaifa ya Bustani ya Wanyama na Uhifadhi wa Biolojia ya Smithsonian (NZCBI) imesema kuwa Panda Bao Li, jike mwenye umri wa miaka miwili ambaye jina lake linatafsiriwa kwa Kiingereza kama "hazina" na "mwenye nguvu," ataingia kwenye bustani hiyo ya wanyama baadaye mwaka huu.
Bao Li ni mtoto wa Panda Bao Bao na kijukuu cha Tian Tian na Mei Xiang. Bao Bao, Tian Tian na Mei Xiang wote wamewahi kuishi kwenye bustani hiyo ya wanyama hapo awali, na Bao Bao alizaliwa huko.
Pia panda mwingine atakayewasili baadaye mwaka huu ni Qing Bao, panda jike mwenye umri wa miaka miwili. Jina lake linamaanisha "kijani" na "hazina" kwa lugha ya Kichina.
NZCBI pia imetangaza kwamba imeongeza muda wa makubaliano ya ushirikiano wa utafiti na uzalianaji wa panda na Shirikisho la Uhifadhi wa Wanyamapori la China, mpaka Aprili 2034. Makubaliano hayo yatazifanya Marekani na China kuendeleza ushirikiano wao katika kuhifadhi spishi za panda.
"Leo, ninafuraha sana kuchangia nanyi baadhi ya habari njema: Bao Li na Qing Bao, balozi wetu mpya wa urafiki, hivi karibuni watapita (Bahari ya) Pasifiki na kujiunga na familia kubwa ya Bustani ya Kitaifa ya Wanyama," Balozi wa China nchini Marekani Xie Feng amesema katika hotuba yake kwenye hafla iliyoandaliwa na bustani hiyo ya wanyama.
Balozi Xie amesema mafanikio ya China katika kuhifadhi panda "hayatenganishwi na ushirikiano wa kimataifa," ikiwa ni pamoja na Marekani, ambayo ni "miongoni mwa nchi za kwanza" kushirikiana na China na kufanya jitihada za pamoja za kuokoa wanyama hao waliokuwa katika hatari ya kutoweka.
"Tunafuraha kutangaza ukurasa unaofuata wa ushirikiano wetu wa uzalianaji na uhifadhi unaanza kwa kuwakaribisha panda wawili wapya, ikiwa ni pamoja na mzao wa familia yetu tuipendayo ya panda, hapa Washington, D.C.," amesema Brandie Smith, Mkurugenzi wa idara ya John na Adrienne Mars ya NZCBI.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma