Xi Jinping atoa wito wa juhudi zaidi za kujenga jumuiya ya China na Nchi za Kiarabu yenye mustakabali wa pamoja (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 31, 2024
Xi Jinping atoa wito wa juhudi zaidi za kujenga jumuiya ya China na Nchi za Kiarabu yenye mustakabali wa pamoja
Rais Xi Jinping wa China akihudhuria hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 10 wa mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu na kutoa hotuba kuu kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai mjini Beijing, China, Mei 30, 2024. (Xinhua/Yin Bogu)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Alhamisi alipokuwa akitoa hotuba yake kuu ya ufunguzi wa mkutano wa 10 wa mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu (CASCF) ametoa wito kwa China na Nchi za Kiarabu kuzidisha ushirikiano na kuongeza kasi ya ujenzi wa Jumuiya ya China na Nchi za Kiarabu yenye mustakabali wa pamoja.

Uhusiano wa China na Nchi za Kiarabu wapanda ngazi mpya

Uhusiano kati ya China na nchi za Kiarabu umeendelea kupanda ngazi mpya tokea karne mpya. Kwenye Mkutano wa kwanza wa wakuu wa China na nchi za Kiarabu mjini Riyadh, Saudi Arabia, mwezi Desemba 2022, China na nchi za Kiarabu zilikubaliana kujenga jumuiya ya China na Nchi za Kiarabu yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.

Rais Xi amesema kuwa China imeridhishwa na mafanikio ambayo yamepatikana katika kufanikisha matokeo ya Mkutano wa kwanza wa wakuu wa China na nchi za Kiarabu. Amesema, China itashirikiana pamoja na nchi za Kiarabu katika kuongeza umuhimu wa mkutano huo wa kutoa mwongozo wa kimkakati kwa ajili ya kuendeleza "ukuaji wa kasi" wa uhusiano kati ya China na Nchi za Kiarabu.

Ametangaza kuwa China itakuwa mwenyeji wa mkutano wa pili wa wakuu wa China na Nchi za Kiarabu Mwaka 2026, ambao utakuwa mnara nyingine wa uhusiano kati ya China na nchi za Kiarabu.

Rais Xi amesema China itashirikiana na nchi za Kiarabu kuufanya uhusiano kati ya China na nchi za Kiarabu kuwa mfano wa kulinda amani na utulivu wa dunia , kuwa kielelezo cha ujenzi wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kuwa mfano wa kuigwa kwa kuishi kwa mapatano kati ya ustaarabu mbalimbali, na kuwa mfano wa kutafuta njia sahihi ya usimamizi wa Dunia.

Mifumokazi mitano ya ushirikiano

Katika mkutano wa kwanza wa wakuu wa China na Nchi za Kiarabu mwaka 2022, Rais Xi alitoa "mipango minane mikuu ya ushirikiano" kwa ajili ya ushirikiano wenye matokeo halisi.

Mavuno ya mapema yamepatikana katika "mipango yote minane mikuu ya ushirikiano," Rais Xi amesema, huku akiongeza kuwa China ingependa kushirikiana na upande wa Nchi za Kiarabu kwenye msingi huo kwa kuweka "mifumokazi mitano ya ushirikiano" ili kuongeza ujenzi wa Jumuiya ya China na Nchi za Kiarabu yenye mustakabali wa pamoja.

Mifumokazi hiyo mitano inajumuisha mfumokazi madhubuti zaidi wa uvumbuzi, mfumokazi unaopanuliwa wa uwekezaji na ushirikiano wa mambo ya fedha, mfumokazi unaohusisha nyanja nyingi zaidi wa ushirikiano wa nishati, mfumokazi wenye usawa zaidi wa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara wenye kunufaishana, na mfumokazi mpana zaidi wa mabadilishano kati ya watu.

Kushikilia suluhu ya Nchi Mbili

Mashariki ya Kati ni ardhi iliyobarikiwa matarajio mapana ya maendeleo, lakini vita bado vinaendelea juu yake. Tangu Oktoba mwaka jana, mgogoro wa Palestina na Israel umezidi kuwa hali mbaya, na kuingiza watu katika mateso makubwa, Rais Xi amesema.

Amesisitiza kuwa vita havipaswi kuendelea kwa muda usio na ukomo, haki haipaswi kukosekana milele, na dhamira ya suluhu ya Nchi Mbili isiyumbishwe ovyo.

Amesema, China inaunga mkono kithabiti uanzishwaji wa Nchi huru ya Palestina yenye mamlaka kamili kwenye msingi wa mipaka ya Mwaka 1967 na Jerusalem Mashariki ikiwa mji mkuu wake.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha