“Mashine ya kujenga majengo” yawezesha ujenzi wa majengo wa kutumia akili mnemba mkoani Shandong, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 31, 2024
“Mashine ya kujenga majengo” yawezesha ujenzi wa majengo wa kutumia akili mnemba mkoani Shandong, China
Mfumo wa roboti ya kujenga majengo ya makazi wa “Tianchan” ukitumika kwenye mradi wa kuboresha mtaa wa makazi duni wa Mji wa Jiaozhou wa Qingdao, China. (Picha imepigwa tarehe 29, Mei)

Hivi karibuni, mfumo wa roboti ya kujenga majengo ya makazi wa “Tianchan” uliovumbuliwa kwa kujitegemea na Idara ya Nane ya Kampuni ya Ujenzi ya China (China Construction Eighth Engineering Division, CCEED) umeanza kutumika kwenye Mji wa Qingdao, Mkoa wa Shandong wa China.

Inafahamika kuwa, mashine hiyo ya kujenga majengo inafungamanisha sifa za ujenzi wa kutumia akili mnemba na wa kijani, ikiwa na faida ya ujenzi wenye ufanisi, salama, na wenye kuaminika, gharama nafuu na kiwango kinachodhibitika. Mfumo wa “Tianchan” unaweza kukamilisha ujenzi wa ghorofa moja ndani ya siku tano, idadi ya wafanyakazi hupunguzwa kwa nusu, na muda wa ujenzi hufupishwa kwa theluthi.

(Picha na Li Ziheng/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha