

Lugha Nyingine
Mwendesha wa kike wa mashine za kilimo asaidia wanakijiji kwa kuendesha mashine ya kuvuna mazao
Huku kukiwa na mawimbi ya dhahabu ya ngano na kuunguruma kwa mashine za kilimo, mwendesha mashine wa kike Du Mengyuan mwenye umri wa miaka 22, anaendesha kwa ustadi mashine mchanganyo ya kuvuna mazao kupita shambani.
Akiwa alikulia katika kijiji cha mashambani, Du Mengyuan amekuwa na uhusiano wa kina na ardhi hiyo. Baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu Mwaka 2023, alifanya uamuzi kwa ujasiri kurudi kijiji kwao alikozaliwa na kuanzisha shughuli zake mwenyewe. "Ninapenda ardhi hii na ninatumai kusaidia kijiji changu kwa kutumia yale niliyopata katika masomo yangu ," Du amesema.
Katika mwaka mmoja uliopita, Du ametumia majukwaa ya mtandaoni kuuza bidhaa za kienyeji za kilimo, huku pia akinasa msingi wa maisha ya kijijini kupitia kamera yake wakati wa mapumziko. Mwezi Aprili mwaka huu, Du alipata mafanikio makubwa alipopata leseni yake ya kuendesha gari ya trekta na mashine mchanganyo ya kuvuna mazao.
"Siku chache zilizopita zimekuwa za shughuli nyingi sana. Sina muda wa kula, na simu yangu inaendelea kuita kwa oda za kuvuna mazao," Du amesema. "Kila siku, mimi hukimbia huku na huko kusaidia wanakijiji mavuno yao ya ngano. Inachosha, lakini inanipa hisia kubwa ya kufanikiwa."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma