Maonesho ya Ndege za Kusafiri Kimo cha Chini yasaidia Guangzhou kujenga mji wa kwanza nchini China wa uendeshaji wa kibiashara wa safari za ndege hizo za abiria

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 04, 2024
Maonesho ya Ndege za Kusafiri Kimo cha Chini yasaidia Guangzhou kujenga mji wa kwanza nchini China wa uendeshaji wa kibiashara wa safari za ndege hizo za abiria
Picha ikionesha ndege ya kubeba abiria ya eVTOL “Shengshilong” kwenye Maonesho ya Ndege za Kusafiri Kimo cha Chini ya Guangzhou. Ndege hiyo ina muundo wa viti vitano, uwezo wa kuruka kwa kubeba uzito wa tani 2, na kasi ya zaidi ya kilomita 200 kwa saa. (Picha imepigwa tarehe 1, Juni)

Hivi karibuni, Maonyesho ya Ndege za kusafiri Kimo cha Chini yamefanyika kwenye uwanja wa Majengo ya Tianhe katika Mji wa Guangzhou, China ambapo aina zaidi ya kumi za ndege maarufu za eVTOL (ndege za kutumia nishati ya umeme za kuruka na kutua wima) zilionyeshwa kwa mara ya kwanza. Mji huo wa Guangzhou hivi karibuni umetoa "Mpango wa Utekelezaji wa Maendeleo ya Uchumi wa Kimo cha Chini wa Mji Guangzhou". Maonyesho hayo ni hatua ya kampuni za mji huo zinazojishughulisha na uchumi wa kimo chini, na yanasaidia Guangzhou kuwa mji wa kwanza nchini China unaoendesha usafiri wa kibiashara wa kubeba abiria kwenye urefu wa kimo cha chini.

(Picha na Liu Dawei/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha