Claudia Sheinbaum atangazwa mshindi katika uchaguzi wa urais wa Mexico (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 04, 2024
Claudia Sheinbaum atangazwa mshindi katika uchaguzi wa urais wa Mexico
Claudia Sheinbaum akijiandaa kupiga kura kwenye kituo cha kupigia kura huko Mexico City, Mexico, Juni 2, 2024. (Xinhua/Li Muzi)

MEXICO CITY - Mwanasayansi wa tabianchi wa Mexico na meya wa zamani wa Mexico City Claudia Sheinbaum amesherehekea ushindi wake katika uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili akiwa mgombea wa muungano wa "Let's Keep Making History" ambapo Sheinbaum, mwenye umri wa miaka 61, sasa atakuwa rais wa kwanza mwanamke wa Mexico katika kipindi cha zaidi ya miaka 200 tangu nchi hiyo ipate uhuru wake.

Sheinbaum alitoa hotuba ya kukubali ushindi wake asubuhi ya Jumatatu baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Mexico kutangaza matokeo ya uchaguzi kwa mchakato wake wa kuhesabu kura kwa haraka. Matokeo ya awali yalionyesha kuwa alikuwa ameshinda kwa kupata kati ya asilimia 58.3 na asilimia 60.7 ya kura zote halali zilizopigwa.

Mgombea wa upinzani Xochitl Galvez amepata kati ya asilimia 26.6 na 28.6 ya kura, na kukubali kushindwa na mpinzani wake huyo wa chama tawala Sheinbaum siku ya Jumatatu.

Mgombea pekee mwanamume katika uchaguzi huo, Jorge Alvarez Maynez, aliyegombea kwa tiketi ya chama cha Vuguvugu la Wananchi, Citizens' Movement, amepata kati ya asilimia 9.9 na 10.8 ya kura zote halali. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha