Reli ya metro iliyojengwa na China yatoa huduma ya safari ya kufurahisha na ya starehe katika mji mkuu wa Nigeria (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 05, 2024
Reli ya metro iliyojengwa na China yatoa huduma ya safari ya kufurahisha na ya starehe katika mji mkuu wa Nigeria
Wafanyakazi wa reli ya metro ya Abuja wakiwa katika picha ya pamoja kwenye behewa la treni mjini Abuja, Nigeria, Mei 23, 2024. (Xinhua/ Yan Yujuan)

ABUJA - Akihisi mshindo laini wa treni chini yake, James Anowai, mtayarishaji maudhui na MwanaYouTube, alikuwa katika msisimko wa furaha wakati akiwa ametulia katika kiti chake kwenye Usafiri wa Umma wa Reli ya Abuja (ARMT) ulioboreshwa katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja hivi karibuni.

Kwa Anowai, ambaye shauku yake ilikuwa dhahiri, safari hii haikuwa tu mara yake ya kwanza ya kupanda treni au kufanya safari kutoka kituo kimoja hadi kingine bali pia ni fursa ya kueleza jambo jipya na la kusisimua na wafuatiliaji wake wa mtandaoni kuhusu reli nyepesi ya Abuja iliyojengwa na Shirika la Ukandarasi wa Ujenzi la China, ambalo ni shirika kubwa la ujenzi wa kimataifa la China.

"Kila mtu ametulia vizuri. Ni laini sana, safi, na kwa kweli, safari nzuri. Ni jambo ambalo ninataka kufanya tena na tena," ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano, akinasa nyakati hizo nzuri kwenye camera ya simu yake.

Tangu kuzinduliwa kwake upya kwa shughuli za kibiashara wiki takriban moja iliyopita, mazungumzo kuhusu ARMT yamekuwa yakiendelea, huku vyombo vya habari vya Nigeria vikiwa na matazamio ya mfumo huo wa reli nyepesi katika mji mkuu huo unaoendelezwa kwa kasi wa Nigeria.

Katika hafla ya kuanzisha shughuli za kibiashara za reli hiyo iliyofanyika Mei 29, Rais Bola Tinubu wa Nigeria alitangaza kwamba safari kwenye mfumo huo mpya wa metro itakuwa bure hadi mwisho wa mwaka huu -- hatua ambayo inatarajiwa kuhimiza wakaazi kukumbatia njia hii mpya ya usafiri na kupunguza mizigo yao ya kiuchumi.

Rais Tinubu, ambaye alipanda treni pamoja na maofisa wengine wakuu, alielezea uendeshaji wa huduma za usafiri kwenye njia hiyo ya metro ya Abuja kama "hatua muhimu ya maendeleo ya kudumu kama nchi na katika Eneo la Makao Makuu ya Serikali Kuu (FCT)," huku akibainisha kuwa imekuwa ikiwa ni "matunda ya ushirikiano, kudhamiria, maendeleo, na kuona mbele."

Sehemu iliyokamilishwa ya urefu wa kilomita 45 ya Loti A1 na 3 ya reli hiyo nyepesi, yenye urefu wa kilomita 290 ikitoa huduma ya usafiri wa umma ndani ya jiji na kuunganisha miji karibu na jiji la Abuja, ni sehemu ya mradi wa usafiri wa umma wa reli ya Abuja iliyoundwa kuwa na muunganisho na njia ya taifa katika pointi mbili, ambapo kutakuwa na miingiliano ya kuunganisha njia ya reli inayounganisha sehemu ya kaskazini ya Nigeria.

Reli hiyo ina stesheni 12, ofisi 21 za uendeshaji, madaraja 13, kalveti 50, na madaraja tisa ya kuvusha waenda kwa miguu. Ujenzi wa reli hiyo nyepesi na matumizi yake unatarajiwa kufungua miji mipya na kukuza shughuli za kiuchumi kwenye ukanda wa Gwagwa, Kalgoni, Dei-Dei, Kubwa, Kukwaba, Dasonga, Asa, kati ya miji midogo 12 karibu na mji mkuu wa Nigeria, Abuja.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha