Wanawake wa Uganda wageuza taka za kilimo kuwa nishati ya baiolojia ili kuokoa miti

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 06, 2024
Wanawake wa Uganda wageuza taka za kilimo kuwa nishati ya baiolojia ili kuokoa miti
Sheeba Kwagala (Kulia) na mwenzake Shadia Abasa wakitumia vitu mbalimbali kutengeneza briketi kwenye kambi mjini Kampala, Uganda, Mei 30, 2024. (Picha na Nicholas Kajoba/Xinhua)

KAMPALA - Kila asubuhi, Sheeba Kwagala na mwenzake wanaelekea kwenye kambi katika mji mkuu wa Uganda Kampala kuponda taka za kilimo, hasa maganda ya ndizi na mabaki ya mazao, pamoja na molasi na udongo ili kutengeneza briketi.

Briketi, ambayo ni aina ya chanzo cha nishati mbadala na aina ya nishati yabisi ya baiolojia, ina ufanisi bora wa nishati kuliko kuni au mkaa, ambayo hutumiwa kwa kiasi kikubwa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

"Tunaponda taka za kilimo, kisha tunachanganya na udongo na molasi ili kuifanya kuwa yabisi. Tunaweka vitu mbalimbali kwenye mashine inayounda briketi. Kujifunza jinsi ya kutengeneza briketi ni rahisi, na nitachangia ujuzi wangu na wanawake wengine," Kwagala mwenye umri wa miaka 20, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), nishati ya baiolojia ndiyo chanzo kikuu cha nishati nchini Uganda, ikichukua asilimia 94 ya nishati yote inayozalishwa. Kati ya jumla ya nishati ya baiolojia inayotumiwa, kuni huchukua asilimia takriban 80, mkaa asilimia 10, na mabaki ya mazao asilimia 4. Kaya tisa kati ya 10 hutumia kuni au mkaa kupikia.

FAO imebainisha kuwa matumizi ya mkaa una athari mbaya sana za kimazingira, kijamii na kiuchumi.

Licha ya ongezeko la hivi karibuni la misitu kutoka asilimia 9 Mwaka 2015 hadi asilimia 13 Mwaka 2021, huku ikitarajiwa kupanda hadi asilimia 15 ifikapo 2025, misitu ya Uganda ilipungua kutoka asilimia 25 ya ardhi ya nchi hiyo Mwaka 1990 hadi asilimia karibu 9 Mwaka 2015, kwa mujibu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Misitu ya Uganda, ambayo ni shirika la serikali la uhifadhi wa misitu nchini Uganda.

Wakati dunia ilipoadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, ambayo hufanyika Juni 5 kila mwaka, Kwagala na idadi inayoongezeka ya watengeneza briketi nchini Uganda wanaleta mabadiliko. Kupitia shirika lao la uangalizi, Set Her Free, ambayo ni shirika lisilo la kiserikali la eneo hilo linayowawezesha wanawake vijana walio katika mazingira magumu, wanatoa matofali kwenye migahawa, shule na taasisi nyingine ambazo zinahama kutoka kwenye matumizi ya kuni au mkaa kama nishati.

Michael Kalyesubula, mpishi katika mgahawa mmoja mjini Kampala, ameliambia Xinhua kwamba sasa anapendelea kutumia briketi badala ya mkaa. "Kama tunakula chakula kilichopikwa kwa mkaa, ambayo ina athari mbaya kwa mazingira, siyo sawa. Baada ya kuanza kutumia briketi, tumeanza kuelewa kuwa zinatusaidia kuokoa mazingira."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha