Daraja Kubwa la Mozhai Wujiang la sehemu ya nyongeza ya Barabara kuu ya Chongqing-Hunan ya China kuunganishwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 11, 2024
Daraja Kubwa la Mozhai Wujiang la sehemu ya nyongeza ya Barabara kuu ya Chongqing-Hunan ya China kuunganishwa
Picha iliyopigwa tarehe 9, Juni ikionesha sehemu ya ujenzi wa Daraja Kubwa la Mozhai Wujiang la sehemu ya nyongeza ya Barabara kuu ya Chongqing-Hunan ya China.

Siku hizi, daraja kubwa la Mozhai Wujiang la sehemu ya nyongeza ya Barabara kuu ya Chongqing-Hunan lililopo mji wa Chongqing, China limefikia hatua ya mwisho ya ujenzi wa nguzo, likikaribia muda wake wa kuunganishwa.

Daraja hilo liliwekezwa na kampuni ya uwekezaji ya Chongqing ya Kundi la Ujenzi wa Reli la China, na kujengwa na kampuni ya bandari na usafiri wa majini ya kundi hilo. Daraja hilo lina urefu wa mita 708 na kuvuka mita 296.

Sehemu ya nyongeza ya Barabara kuu ya Chongqing-Hunan ya China ina urefu wa kilomita 280, ikitarajiwa kuzinduliwa rasmi mwaka 2025.

(Picha na Tang Yi/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha