Sehemu mbalimbali nchini China zawapokea watalii wa nchini milioni 110 wakati wa likizo ya Sikukuu ya Duanwu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 11, 2024
Sehemu mbalimbali nchini China zawapokea watalii wa nchini milioni 110 wakati wa likizo ya Sikukuu ya Duanwu
Picha iliyopigwa tarehe 10, Juni, 2024 ikionesha watalii wakitembelea Ziwa Shouxihu huko Yangzhou, Mkoa wa Jiangsu wa China. (Picha na Zhou Shegen/Xinhua)

Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China Jumatatu ilisema kuwa, wakati wa likizo ya Sikukuu ya Duanwu, sehemu mbalimbali nchini China waliwapokea watalii wa nchini milioni 110 kwa jumla, idadi iliyoongezeka kwa asilimia 6.3 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Takwimu za wizara hiyo zimeonesha kuwa, katika likizo hiyo (kuanzia Jumamosi hadi Jumatatu), matumizi ya watalii wa nchini China yalifikia Yuan bilioni 40.35 (takriban dola bilioni 5.57 za Marekani), ikiongezeka kwa asilimia 8.1 kuliko kipindi kama hicho mwaka jana.

Watalii nchini China wanapendelea zaidi kufanya utalii kwa njia mbalimbali tofauti ambazo zinafuata tabia zao wenyewe. Mikoa ya Yunnan, Qinghai, Gansu, Mongolia ya Ndani na Guizhou imependelewa zaidi na watalii vijana. Wizara ya Utalii na Utamaduni ilisema, maeneo haya yanafaa hasa kwa safari za kuendesha gari na za kuepuka joto.

Sikukuu ya Duanwu ni sikukuu ya jadi ya China. Sikukuu hiyo ya kila mwaka ni siku ya tano ya mwezi wa tano kwa kalenda ya jadi ya China. Mwaka huu, Sikukuu ya Duanwu ilikuwa Jumatatu wiki hii.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha