Hali mbaya ya hewa yaifanya China kukabiliwa na joto na dhoruba kali za mvua

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 12, 2024
Hali mbaya ya hewa yaifanya China kukabiliwa na joto na dhoruba kali za mvua
Watu wakiwa wamekaa chini ya hema ili kujikinga na jua kali kwenye Bustani ya Chaoyang mjini Beijing, China, Juni 9, 2024. (Xinhua/Chen Zhonghao)

BEIJING - Wakati eneo la kaskazini ya China likiwa linakabiliwa na wimbi la joto kali na hali joto za kila siku inavyovunja rekodi, dhoruba za mvua zinatabiriwa kukumba maeneo mengi ya ngazi ya mkoa katika kusini mwa China, zikiongeza kutolewa kwa tahadhari nyingi nchini kote.

Saa 12 asubuhi siku ya Jumanne, Kituo cha Kitaifa cha Hali ya Hewa cha China (NMC) kilitoa tahadhari ya halijoto ya juu ya rangi ya chungwa, ambayo ni daraja la pili la juu zaidi katika mfumo wa tahadhari wa China, kikitabiri hali joto ya juu ya mchana katika mikoa na maeneo yakiwemo Beijing, Tianjin, Hebei, Henan, Shangdong na Xinjiang, na mengine. Halijoto katika baadhi ya sehemu za mikoa ya Hebei na Xinjiang huenda ikapita nyuzi joto 40.

Katika Mkoa wa Hebei wa kaskazini mwa China, kituo cha uchunguzi wa hali ya hewa cha mkoa huo kimetoa tahadhari nyekundu ya hali joto ya juu siku ya Jumanne, saa 11 asubuhi, kikisema kuwa vituo vingi vya hali ya hewa katika eneo linaloanzia sehemu za kusini za Mji wa Baoding hadi miji ya Xingtai na Handan vinaweza kushuhudia hali yao ya hewa ya joto zaidi vikiwa na hali joto inayozidi nyuzi joto 40.

Beijing, mji mkuu wa China, pia umekumbwa na wimbi la joto la siku 3 kuanzia Jumanne.

Kamati ya Elimu ya Beijing imependekeza kuwa shule za chekechea, shule za msingi na sekondari na shule za kazi za ufundi zipunguze madarasa ya nje ya elimu ya viungo na shughuli za nje.

Kwa mujibu wa utabiri uliochapishwa na NMC, halijoto za juu zinatazamiwa kuongezeka kaskazini mwa China. Maeneo ya kati na kusini ya kaskazini mwa China, sehemu kubwa ya maeneo ya Mto Manjano na Mto Huaihe , kusini mwa Shanxi, na eneo la Guanzhong mkoani Shaanxi yanatazamiwa kukumbwa na hali joto za siku 6 hadi 8 zinazozidi nyuzi joto 35. Baadhi ya maeneo ya Henan yanaweza kushuhudia siku 9 hadi 10 za halijoto hiyo ya juu.

Katika kipindi hicho, hali joto za kila siku katika baadhi ya maeneo ya Hebei, Henan, Shanxi na Shandong zinaweza kufikia au kuzidi rekodi za kihistoria kwa kipindi hicho, imesema NMC.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha