Panda mashuhuri Fu Bao asalimia watembeleaji kwa mara ya kwanza mkoani Sichuan, China tangu atoke Jamhuri ya Korea (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 13, 2024
Panda mashuhuri Fu Bao asalimia watembeleaji kwa mara ya kwanza mkoani Sichuan, China tangu atoke Jamhuri ya Korea
Panda Fu Bao akila chakula kwenye boma lake katika kituo cha panda cha Shenshuping cha Bustani ya Kitaifa ya Mazingira Asilia ya Wolong, Mkoa wa Sichuan, Kusini-Magharibi mwa China, Juni 12, 2024. (Xinhua/Shen Bohan)

CHENGDU - Fu Bao, panda wa kwanza kuzaliwa katika Jamhuri ya Korea (ROK), amekutana na watembeleaji siku ya Jumatano asubuhi baada ya kurejea katika Mkoa wa Sichuan, China, mji wa nyumbani kwa panda ambapo makumi ya wageni na vyombo vya habari vya kimataifa vilimngojea panda huyo mashuhuri kabla ya Fu Bao kuingia kwenye ua wa boma lake katika kituo cha panda cha Shenshuping cha Bustani ya Kitaifa ya Mazingira Asilia ya Wolong saa 3:35 asubuhi (kwa saa za Beijing), kufuatia miezi miwili ya ukaguzi, karantini na kuzoea hali ya mazingira mapya.

Alikuwa akitembea polepole, akinusa na kutazama huku na huko kwa hamu. Baada ya kuchunguza uwanja wake, alipata chakula kilichotayarishwa kwa ajili yake kwenye uwanja wa kuchezea, ambapo alijivinjari kwenye karamu ya michipukizi ya mianzi.

Cheng Jianbin, mhifadhi wa Fu Bao amesema, panda huyo alikuwa akilishwa mianzi ya kilo 30 hadi 40 kila siku, pamoja na kilo tano hadi 10 za machipukizi ya mianzi. Madaktari wa wanyama na wahifadhi hufuatilia kiasi cha chakula chake, haja kubwa na hali ya kiakili ili kuhakikisha panda huyo anaishi maisha ya starehe.

Li Desheng, naibu mkurugenzi wa Kituo cha Uhifadhi na Utafiti wa Panda cha China, amesema kuwa uzito wa Fu Bao ni uthibitisho wa kuzoea haraka mazingira mapya. "Umekuwa kati ya kilo 103 na 106 katika kipindi cha miezi miwili iliyopita," amesema. "Ni sawa na uzito wake wakati yuko Jamhuri ya Korea, na ndani ya kiwango cha kawaida cha panda katika kundi la panda wenye umri huo."

Fu Bao alirejea China mapema Aprili. Wei Rongping kutoka kituo cha Shenshuping amebainisha kuwa changamoto kubwa kwake ilikuwa namna ya kuweza kujumuika na "familia ya panda" huko.

Akiwa alizaliwa Julai 2020, Fu Bao ambayo inamaanisha "hazina ya bahati" kwa Kiingereza, ni mtoto wa kwanza wa panda Ai Bao na Le Bao, ambao walitumwa Jamhuri ya Korea kutoka China Mwaka 2016 kwa kukodishwa kwa miaka 15. Kwa haraka alianza kuvuma mtandaoni miongoni mwa watumiaji wa mtandao huko Jamhuri ya Korea baada ya kuzaliwa, na kuwa chanzo cha furaha kwa watu wakati wa janga la UVIKO-19.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha