Mfereji Mkuu waleta uhai mpya kwa utamaduni na utalii wa Mji wa Hangzhou, China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 14, 2024
Mfereji Mkuu waleta uhai mpya kwa utamaduni na utalii wa Mji wa Hangzhou, China
Picha iliyopigwa tarehe 12 Juni 2024 ikionyesha Mtaa wa Qiaoxi wa kihistoria na kitamaduni kando ya Mfereji Mkuu mjini Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China. (Xinhua/Weng Xinyang)

Mfereji Mkuu unaounganisha Mji wa Beijing na wa Hangzhou mkoani Zhejiang, Mashariki mwa China, umekuwa na historia ya zaidi ya miaka 2500, ulitumika kama ateri muhimu ya mawasiliano katika zama za kale za China. Mfereji huo uliorodheshwa kuwa mali ya Urithi wa Dunia na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) Juni 2014.

Miaka ya hivi karibuni, serikali za mitaa za sehemu mbalimbali nchini China zimeweka mkazo katika ulinzi wa eneo hilo huku zikiendeleza ulinzi wa mali ya urithi wa kitamaduni kila wakati, utumiaji tena wa mabaki ya viwanda na urithi wa utamaduni usioshikika, hatua kwa hatua zikijenga kando za Mfereji Mkuu huo kuwa eneo linalojumuisha tamaduni tajiri, mazingira mazuri na utalii unaostawi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha