Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Fujian zasababisha watu kuondoka kwenye makazi yao

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 17, 2024
Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Fujian zasababisha watu kuondoka kwenye makazi yao
Waokoaji wakikagua hali ya mafuriko kwenye mfereji wa maji katika Kijiji cha Hongxing cha Tarafa ya Xingcun ya Wuyishan ya Mji wa Nanping, Mkoa wa Fujian, Kusini Mashariki mwa China, Juni 16, 2024. (Picha na Chen Ying/Xinhua)

FUZHOU - Mvua kubwa inayoendelea kunyesha imesababisha watu 36,000 wa Mkoa wa Fujian, Mashariki mwa China kuondoka kwenye makazi yao, idara ya udhibiti wa mafuriko ya mkoa huo imesema siku ya Jumapili kwamba, mvua kubwa iliyoendelea kunyesha imeleta uharibifu mkubwa katika maeneo mengi ya mkoani Fujian, mkoa huo umetangaza mwitikio wa dharura kwa dhoruba hiyo ya mvua.

Hadi saa 2 usiku siku ya Jumamosi, duru mpya ya mvua imeathiri watu 179,800 na kuharibu hekta 12,350 za mashamba ya mazao, na kusababisha hasara ya moja kwa moja ya kiuchumi yenye thamani ya Yuan bilioni 1.61 (kama dola za Kimarekani milioni 225), idara hiyo imesema.

Kuanzia saa 12 asubuhi siku ya Jumamosi hadi saa 1 asubuhi siku ya Jumapili, baadhi ya vituo vya kupima viwango vya maji katika mito 11 mkoani Fujian vilikuwa vimeripoti viwango vya maji kati ya mita 0.07 na mita 3.65 juu ya kiwango cha tahadhari, idara hiyo imebainisha.

Kufikia saa 1 asubuhi Jumapili, viwango vya maji katika vituo saba vya kupima viwango vya maji vilikuwa vimeendelea kuwa juu ya kiwango cha tahadhari.

Huang Zhigang, mtaalamu wa idara ya hali ya hewa ya Fujian, amewataka watu kuwa waangalifu kutokana na hatari ya mafuriko katika mito midogo na ya kati na uwezekano wa kujaa maji katika maeneo ya mijini na vijijini. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha