Meli ya hospitali ya Kikosi cha Majini cha Jeshi la China (PLA) yaanza safari ya kikazi Mwaka 2024 (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 17, 2024
Meli ya hospitali ya Kikosi cha Majini cha Jeshi la China (PLA) yaanza safari ya kikazi Mwaka 2024
Wanajeshi wa meli ya hospitali ya Kikosi cha Majini cha Jeshi la China (PLA) ya "Peace Ark" wakishiriki zoezi la uokoaji kabla ya kuanza safari ya kikazi ya Mapatano-2024, Juni 1, 2024. (Liu Zhilei/Xinhua)

HANGZHOU - Meli ya hospitali ya Kikosi cha Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) ya "Peace Ark" imeng’oa nanga kutoka bandari ya kijeshi huko Zhoushan, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China siku ya Jumapili asubuhi kwa ajili ya safari ya kikazi wa Mapatano-2024 ambapo wakati wa safari yake hiyo, itatembelea nchi 13, ambazo ni Ushelisheli, Tanzania, Madagascar, Msumbiji, Afrika Kusini, Angola, Jamhuri ya Kongo, Gabon, Cameroon, Benin, Mauritania, Djibouti na Sri Lanka, na kutoa huduma za matibabu kwa watu wenyeji. Pia itatembelea bandari za Ufaransa na Ugiriki.

Hiyo ni safari ya 10 ya kikazi kwa meli hiyo ya "Peace Ark" tangu kuanzishwa kwake Mwaka 2008. Meli hiyo ya "Peace Ark" itatoa huduma za upimaji, utambuzi na matibabu ya magonjwa ya kawaida na ya maambukizi bila malipo kwa wakazi wenyeji, watu katika makampuni ya China, na Wachina wanaoishi nchi za nje kupitia kliniki za ndani ya meli na timu za madaktari ambazo zimetumwa katika nchi husika.

Kuna wataalamu zaidi 100 ndani ya meli hiyo ya hospitali, wakiwemo wa idara 17 za kliniki na idara 5 za upimaji na utambuzi wa magonjwa.

"Peace Ark” ni meli ya hospitali kwa ajili ya kusafiri kwa umbali baharini ambayo ni ya kwanza kusanifiwa na kuundwa na China. Imeshatembelea nchi na maeneo 45, ikitoa huduma za matibabu kwa watu zaidi ya 290,000.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha