Semina ya maendeleo ya mambo ya Juncao yafanyika Fujian, China (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 17, 2024
Semina ya maendeleo ya mambo ya Juncao yafanyika Fujian, China
Wageni wakihudhuria semina kuhusu maendeleo ya mambo ya teknolojia ya Juncao mjini Fuzhou, Mkoa wa Fujian, Kusini Mashariki mwa China, Juni 16, 2024. (Xinhua/Lin Shanchuan)

Wawakilishi kutoka nchi na maeneo 19 ikiwa ni pamoja na Rwanda, Papua New Guinea, na Fiji, pamoja na wawakilishi wa wataalam, wasomi na kampuni zaidi ya 200 wa China wamehudhuria semina hiyo.

Juncao, ambayo kwa Kichina inamaanisha "uyoga" na "nyasi", inaweza kutumika kukuza uyoga wa chakula na dawa, kama chakula cha mifugo au kama kizuizi cha kijani kudhibiti mmomonyoko wa udongo na kukomesha hali ya kuenea kwa jangwa.

Ikiwa imekita mizizi katika nchi na maeneo zaidi ya 100 duniani kote, Juncao imesifiwa na wenyeji kwa kuiita "nyasi ya Kichina" au "nyasi ya furaha."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha