Habari picha: Askari wa wanyamapori waokoa swala mjamzito wa Tibet wakati wa kuhama mkoani Xizang, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 18, 2024
Habari picha: Askari wa wanyamapori waokoa swala mjamzito wa Tibet wakati wa kuhama mkoani Xizang, China
Picha hii iliyopigwa tarehe 13 Juni 2024 ikionyesha mbwa mwitu katika Hifadhi ya Kitaifa ya Mazingira Asilia ya Qiangtang, Mkoa unaojiendesha wa Xizang, Kusini-Magharibi mwa China. (Jiang Fang/Xinhua)

Siku ya Ijumaa iliyopita, katika sehemu ambayo siyo mbali na kambi ya askari wa wanyamapori iliyoko ndani kabisa ya Hifadhi ya Kitaifa ya Mazingira asilia ya Qiangtang, Mkoa unaojiendesha wa Xizang, Kusini-Magharibi mwa China, mbwa mwitu alimshambulia swala mjamzito wa Tibet kati ya kundi la wanyama hao waliokuwa wakihama, na kumwacha akiwa na majeraha tumboni na shingoni.

Walipomwona swala huyo akihangaika kwenye theluji, askari kadhaa wa wanyamapori walimbeba kumrudisha kambini ili kumwokoa. Kwa bahati mbaya, tumbo lake lilikuwa limepasuliwa, na viungo vya ndani vilikuwa vimeharibiwa zaidi ya kuweza kutibika. Askari hao wa wanyamapori hawakuwa na la kufanya zaidi ya kushona tumbo lake na kumrudisha porini ambapo alikutwa amekufa siku iliyofuata asubuhi.

Kila mwaka, makumi ya maelfu ya swala wajawazito wa Tibet, spishi iliyo chini ya ulinzi wa hali ya juu nchini China, huanza kuhama mwezi wa Mei kwa ajili ya kuzaa na hurudi na ndama wao mwishoni mwa mwezi wa Julai. Maadui wao wa asili wakiwemo mbwa mwitu na dubu huwa muda wote wapo kwa ajili ya kuwavizia. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha