Kuwekeza Xinjiang, China: Gulio Kubwa la Kimataifa laonesha hali motomoto ya mji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 18, 2024
Kuwekeza Xinjiang, China: Gulio Kubwa la Kimataifa laonesha hali motomoto ya mji
Picha ikionesha hali motomto ya mtaa wa chakula wa Gulio Kubwa la Kimataifa la Xinjiang wakati wa usiku. (Picha na Han Ting/People’s Daily Online)

Wakati usiku unapoanza na taa kuwashwa, gulio kubwa la kimataifa la mkoani Xinjiang, China hujaa watu wengi na kuonesha hali motomoto.

Kwenye Mtaa wa chakula wa Gulio Kubwa la Kimataifa la Xinjiang, China ukiwa umezungukwa na taa nzuri za mapambo, sauti za nyimbo za jadi za kabila la Wauygur zinasikika eneo zima, salamu za makaribisho ya wauzaji na mazungumzo ya wateja ni kila mahali, na nyama choma ya mbuzi, kuku pilipili na vyakula vingine mbalimbali vinaonesha picha ya maisha ya usiku ya mji yenye hali motomoto, yakivutia watalii wengi kutoka ndani na nje ya China kwenda huko kutembelea soko hilo la usiku, kuonja chakula kitamu na kujionea uzuri wa Xinjiang.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha