Lugha Nyingine
Jeshi la Israel laidhinisha mipango ya mashambulizi dhidi ya Kundi la Wanamgambo wa Hezbollah la Lebanon (5)
![]() |
| Askari wa akiba wa Israeli akishiriki kwenye mazoezi ya kijeshi huko Kiryat Shmona, Kaskazini mwa Israel, tarehe 18 Juni 2024. (Ayal Margolin/JINI kupitia Xinhua) |
JERUSALEM - Jeshi la Israel limetangaza siku ya Jumanne kwamba limeidhinisha "mipango ya operesheni" kwa ajili ya mashambulizi dhidi ya kundi la wanamgambo wa Hezbollah la Lebanon ambapo katika taarifa yake, jeshi hilo limesema Ori Gordin, kamanda wa Kamandi ya Kaskazini, na Oded Basiuk, mkuu wa Kurugenzi ya Operesheni," wameidhinisha mipango hiyo na kufanya tathmini ya pamoja ya hali ya mambo katika Kamandi ya Kaskazini" ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuendelea na mapambano dhidi ya Kundi la Hezbollah kwenye mpaka wa Israel na Lebanon.
Jeshi hilo limeongeza kuwa "maamuzi hayo yamefanywa juu ya mwendelezo wa kuongeza utayari wa wanajeshi katika uwanja wa mapambano."
Tangazo hilo limekuja wakati ambapo kumekuwa na ongezeko la mvutano kati ya pande hizo mbili, pia wakati ambapo mjumbe maalumu wa Marekani Amos Hochstein, katika ziara yake mjini Beirut, ametoa wito wa kupunguzwa haraka kwa makabiliano kwenye mpaka wa Israel na Lebanon.
Kwenye mkutano wake na viongozi wa Israel siku ya Jumatatu, Hochstein pia amezitaka pande husika kutatua haraka mgogoro kando ya Mstari wa Bluu, ambao ni mpaka kati ya Lebanon na Israel, kupitia njia za kidiplomasia, hali ambayo amesema itaendana na maslahi ya kila upande na "inaweza kufikiwa na ni ya dharura."
Mvutano huo kwenye mpaka wa Israel na Lebanon uliongezeka Oktoba 8, 2023, kufuatia msururu wa makombora yaliyorushwa na Kundi la Hezbollah kuelekea Israel katika kuonesha uungaji mkono kwa mashambulizi ya Kundi la Hamas dhidi ya Israeli siku moja kabla. Kisha Israel ililipiza kisasi kwa kurusha makombora mazito kuelekea kusini mashariki mwa Lebanon.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




