

Lugha Nyingine
Mashabiki wa China waduwazwa na kuwepo kwa matangazo ya kibiashara ya Lugha ya Kichina kwenye Euro 2024 (3)
![]() |
Tangazo la kibiashara la kampuni ya huduma za kufanya malipo mtandaoni ya Alipay ya China likionekana wakati wa mechi ya Kundi D kati ya Austria na Ufaransa ya Kombe la Ulaya mjini Dusseldorf, Ujerumani, Juni 17, 2024. (Xinhua/Ren Pengfei) |
BEIJING - Uwepo matangazo mengi ya kibiashara kwa lugha ya Kichina kwenye Mashindano ya Soka ya Kombe la Ulaya, Euro 2024 hivi karibuni umezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii ya China ambapo ingawa suluhu ya matangazo ya kibiashara ya kidijitali moja kwa moja mtandaoni imetoa mchango, uwepo wa kampuni za China umekuwa ukifuatiliwa sana kwenye Euro 2024 na kampuni tano kati ya jumla ya kampuni wafadhili wakuu 13 wa michuano hiyo zinatoka China.
Watazamaji wa China wamekuwa wakiwekwa katika mazingira ya kutazama matangazo haya ya kibiashara mara kwa mara, kama vile yale ya kampuni ya kuunda magari ya BYD ya China na jukwaa la huduma ya malipo mtandaoni la Alipay, wakati wa matangazo ya moja kwa moja ya mashindano hayo.
Mijadala kuhusu "kampuni za China kwenda kimataifa" imeibuka kwenye jukwaa la mtandao wa kijamii wa Weibo wa China, baada ya kupata watazamaji zaidi ya milioni 100 na makumi ya maelfu ya maoni.
Wachina wengi wamesema kwenye mtandao wa Internet kwamba "kuona kampuni nyingi wanazozifahamu ni kama kutazama Ligi Kuu ya China".
Hii ni mara ya kwanza kwa michuano hiyo kutumia mbinu ya kutangaza matangazo ya kidijitali moja kwa moja mtandaoni katika wakati halisi, ambayo inaweza kubadilisha matangazo kwenye mabango ya LED vinavyozunguka uwanjani kuwa matangazo yanayolenga masoko mahsusi.
Watazamaji wa Ujerumani na Marekani pia wataona matangazo yanayolenga mahususi kwa Lugha za Kijerumani na Kiingereza.
Kwa shirikisho la soka la Ulaya (UEFA), kuanzishwa kwa teknolojia hiyo mpya kumefungua uwezekano mpya wa maendeleo ya soko la Kombe la Ulaya.
Likiwa ni mfadhili mkuu wa Euro 2024, Kampuni ya huduma ya fedha ya China Ant linatangaza chapa kama vile Alipay na Ant Fortune kwa hadhira ya Wachina kwa lugha ya Kichina, huku likitangaza chapa zake za kimataifa za Alipay+, WorldFirst na Antom kwa mashabiki wa kimataifa kwa Lugha ya Kiingereza.
"Hii imejumuishwa katika manufaa yetu ya udhamini na ni chaguo la kawaida kuna chapa tofauti katika masoko tofauti," amesema msemaji kutoka Kampuni za Ant.
Kampuni zisizo wafadhili zinalazimika kununua haki tofauti za utangazaji wa matangazo ya kibiashara kidijitali mtandaoni.
"Hii inaonyesha nguvu ya kifedha ya kampuni za China na umuhimu wa soko la China," mchina mmoja ametoa maoni kwenye mtandao wa Internet.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma