Wapenda michezo wa China washerehekea Siku ya Olimpiki, kukaribisha michezo ya Olimpiki ya Paris (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 24, 2024
Wapenda michezo wa China washerehekea Siku ya Olimpiki, kukaribisha michezo ya Olimpiki ya Paris
Wakazi wa Qingdao, Mkoa wa Shandong, China wakishiriki kwenye shughuli ya kuadhimisha Siku ya Olimpiki, Juni 23, 2024.

NANJING - Mashabiki wa michezo kote nchini China wameadhimisha Siku ya Olimpiki siku ya Jumapili kwa kufanya shughuli mbalimbali za michezo, wakionyesha hamu yao kwa Michezo ijayo ya Olimpiki ya Paris, ambayo itafunguliwa baada ya mwezi mmoja.

Siku ya Olimpiki inalenga kuhimiza ushiriki wa kimataifa katika michezo, bila kujali jinsia, umri au uwezo wa kimichezo. Siku ya Olimpiki ya mwaka huu, yenye kaulimbiu isemayo "Tusonge," ambapo matukio mbalimbali yamefanyika katika miji na maeneo 14 ya China, ikiwemo Beijing, Hangzhou, Nanjing na Qingdao. Maelfu ya watu walishiriki kwenye michezo ya mbio, kambi za utamaduni za Olimpiki na kadhalika.

Kwenye shughuli iliyofanyika mjini Beijing, Zhou Jinqiang, naibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya China, amezungumzia maadhimisho hayo ya kila mwaka ya Siku ya Olimpiki ambayo yamekuwa yakifanyika tangu Mwaka 1987.

"Huku michezo ya Olimpiki ya Paris ikikaribia, wanamichezo wa China wako katika hatua za mwisho za maandalizi. Tunatumai kila mmoja anaweza kushiriki kikamilifu katika michezo, kushangilia wanamichezo wa Olimpiki duniani kote na kufurahia afya na furaha inayoletwa na Michezo ya Olimpiki," Zhou amesema.

Shen Jie, naibu mkurugenzi wa Sekretarieti ya Kamati ya Olimpiki ya China, aliwasilisha ujumbe kutoka kwa Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Thomas Bach, ambaye amewataka watu wahamasishwe katika siku hii maalum, kusherehekea kuzaliwa kwa michezo ya Olimpiki ya kisasa, kuwa na matarajio na Michezo ya Paris, na kufuata kaulimbiu ya Michezo ya Olimpiki, "Haraka zaidi, Juu zaidi, Imara zaidi - Pamoja."

Kote China, wapenda michezo wanakumbatia kikamilifu moyo wa Olimpiki. Huko Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang, wapenda michezo zaidi ya 500 walishiriki katika mbio na kambi za mafunzo ya mpira wa vikapu na soka. Vipindi vya mafunzo ya soka ya bendera, ambao ni mchezo mpya wa Olimpiki, pia vilifanyika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha