

Lugha Nyingine
Wimbi la joto laichoma Marekani, laleta halijoto zinazovunja rekodi (4)
![]() |
Mtoto akipoza mwili kwenye chemchemi katika Kaunti ya Orange, California, Marekani, Juni 22, 2024. (Xinhua) |
LOS ANGELES - Wimbi kubwa la joto limeendelea kutikisa sehemu kubwa ya Marekani wikendi hii, na kusababisha halijoto zinazovunja rekodi na kuweka mamilioni ya watu chini ya tahadhari za joto. Taarifa iliyotolewa na Mfumo Jumuishi wa Kitaifa wa Taarifa za Afya ya Halijoto wa Marekani siku Jumamosi inasema watu zaidi ya milioni 115 kote nchini humo kwa sasa wako chini ya tahadhari zilizotolewa na Idara ya Kitaifa ya Hali ya Hewa ya Marekani (NWS) kuhusu joto kali.
"Wimbi la joto litaendelea kuwepo kwenye sehemu kubwa ya Mashariki ya Marekani iliyopo Kusini ya mpaka moja wa hali ya hewa," Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa cha Marekani (WPC) kimesema Jumamosi.
"Hali za joto hizi zinaendelea kuwa zisizo za kawaida na hatari zaidi kwa msimu wa mapema wa joto katika sehemu za Midwest/Bonde la Ohio mashariki hadi Mid-Atlantic," WPC imesema.
"Hali zitaendelea kuwa za joto kali kutoka katikati hadi kusini mwa California," imesema, na kuongeza kuwa "Jumapili na Jumatatu halijoto hizo zitakuwa juu ya nyuzi za 100 za fahrenheit."
Kuba la joto, lililosababishwa na mfumo wa shinikizo la juu unaonasa hewa joto karibu na ardhini, limetanda sehemu ya Mashariki na Kati na Kaskazini Mashariki mapema wiki hii, likisababisha halijoto zilizovunja rekodi katika miji kadhaa.
Phoenix, mji mkuu wa Jimbo la Arizona, tayari umekuwa siku kadhaa zenye joto kali zaidi za Mwaka 2024 hadi sasa, huku halijoto zikipanda hadi nyuzi joto 115 za fahrenheit wiki hii.
Siku 19 za kwanza za Juni zilikuwa zenye hali joto kali zaidi kwenye rekodi kwa Phoenix. Wastani wa halijoto katika jiji hilo ni nyuzi joto 95.1 za fahrenheit mwaka huu, mwaka wenye hali joto kali zaidi kati ya rekodi za miaka 129, kwa mujibu chombo cha habari cha Familia ya Arizona.
Joto hili kali limesababisha vifo vya watu takriban sita, huku vifo vya watu wengine 87 vikichunguzwa kwa sababu zinazoweza kuhusishwa na joto, imesema Idara ya Afya ya Umma ya Kaunti ya Maricopa katika ripoti iliyotolewa mpya ya uchunguzi wa joto iliyotolewa Juni 15.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma