Rais Xi Jinping asisitiza mambo ya kisasa ya sayansi na teknolojia na uvumbuzi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 25, 2024
Rais Xi Jinping asisitiza mambo ya kisasa ya sayansi na teknolojia na uvumbuzi
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akihudhuria kwenye mkutano wa kitaifa wa sayansi na teknolojia, mkutano wa tuzo ya juu zaidi ya kitaifa ya sayansi na teknolojia, na mkutano wa wataalamu wakuu wa Taasisi kuu ya Sayansi ya China na Taasisi Kuu ya Uhandisi ya China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Juni 24, 2024. (Xinhua/Yao Dawei)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) siku ya Jumatatu amesisitiza umuhimu wa mambo ya kisasa ya sayansi na teknolojia na uvumbuzi katika kutafuta ujenzi wa mambo ya kisasa na maendeleo yenye ubora wa juu ya China.

Akibainisha umuhimu wa sayansi na teknolojia katika uongozi wa kimkakati na utegemeano wa kimsingi, Rais Xi, amehimiza juhudi za kuimarisha mpango wa pamoja kuhusu utendaji wa pande na ngazi mbalimbali na kufanya uratibu wa jumla, na kuharakisha kazi za kujitegemea katika sayansi na teknolojia za kiwango cha juu ili kufikia lengo la kimkakati la kujenga nchi yenye nguvu kisayansi na kiteknolojia ifikapo Mwaka 2035.

Rais Xi ametoa tuzo ya juu zaidi ya sayansi na teknolojia ya China na ametoa maagizo hayo kwenye mkutano wa kitaifa wa sayansi na teknolojia, mkutano wa tuzo ya juu zaidi ya kitaifa ya sayansi na teknolojia, na mkutano wa wataalamu wakuu wa Taasisi Kuu ya Sayansi ya China(CAS) na Taasisi Kuu ya Uhandisi ya China (CAE).

Waziri Mkuu wa China, Li Qiang aliongoza mkutano huo. Naibu Waziri Mkuu, Ding Xuexiang alitangaza uamuzi wa tuzo hiyo. Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi na Li Xi walihudhuria mkutano huo.

Rais Xi ametoa medali na vyeti vya tuzo ya juu zaidi ya sayansi na teknolojia ya China kwa Li Deren, mtaalamu mkuu wa CAS na CAE kutoka Chuo Kikuu cha Wuhan, na Xue Qikun, mtaalamu mkuu wa CAS kutoka Chuo Kikuu cha Tsinghua. Kisha akapeana mikono na wanasayansi hao wawili na kutoa pongezi zake.

Rais Xi na viongozi wengine wa Chama na serikali, pamoja na washindi wawili wa tuzo ya juu zaidi ya sayansi na teknolojia, walitoa vyeti kwa wapokeaji tuzo wengine.

Rais Xi amehimiza kuongeza mafungamano ya pande zote ya uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia na uvumbuzi wa viwandani ili kuhimiza maendeleo ya nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora.

Mikutano hiyo ya Jumatatu ilihudhuriwa na watu takriban 3,000 na kutoa tuzo kwa miradi 250 na wataalamu 12 wa sayansi na teknolojia, huku wanasayansi wawili wakishinda tuzo ya juu zaidi, 49 wameshina Tuzo ya Serikali ya China ya Sayansi ya Asili, 62 wameshinda Tuzo ya Kitaifa ya Uvumbuzi wa Kiteknolojia, 139 wameshinda Tuzo ya Kitaifa ya Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia, na wataalamu 10 wa kigeni wamepata Tuzo ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Sayansi na Teknolojia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha