Baraza la Usalama lasikiliza maelezo ya moja kwa moja ya athari za vita kutoka kwa askari mtoto wa zamani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 27, 2024
Baraza la Usalama lasikiliza maelezo ya moja kwa moja ya athari za vita kutoka kwa askari mtoto wa zamani
Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na migogoro ya kivita ukifanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Juni 26, 2024. (Loey Felipe/Picha ya Umoja wa Mataifa/ Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA - Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesikiliza askari mtoto wa zamani, akifichua ukweli wa kikatili wa vita katika maeneo yenye migogoro kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambapo wakati mtoto huyo wa miaka 16 akizungumza bila kuwekwa wazi utambulisho wake na kupitia mkalimani, amesimulia matukio ya kuhuzunisha ya kutekwa nyara na kulazimishwa kujiunga na kundi lenye silaha.

Mtoto huyo amelitaka baraza hilo kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yenye migogoro ili kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya majanga ya vita.

"Nilizaliwa katika nchi ambayo tayari inakabiliwa na migogoro ya kivita," mtoto alianza. "Nililazimishwa kujiunga na kundi lenye silaha nikiwa njiani ya kwenda shuleni."

Mtoto huyo alisema, miezi miwili iliyopita, mashambulizi ya silaha yalitokea kwenye vijiji vya karibu yakilenga kuwateka nyara watoto, na kuwalazimisha kujiunga kwenye makundi yenye silaha au kuwashikilia kwa ajili ya kupata fedha ya kuwagomboa. Mtoto huyo amesema Shule na hospitali, mara kwa mara zilishambuliwa na kubadilishwa matumizi yake lengwa kuwa vituo vya kijeshi.

Akisimulia mateso ya kibinafsi, mtoto huyo amezungumza juu ya kutekwa nyara na kulazimishwa kujiunga katika kundi lenye silaha, kupitia mateso ya kupigwa, kuporwa, na tisho la kifo.

"Tulilia na kuomba turudi nyumbani, lakini hawakutusikiliza. Walituchapa viboko na kutuweka porini, tukizuiliwa, pamoja na amri ya kumuua yeyote anayejaribu kutoroka," mtoto huyo amekumbuka.

Ameongeza kuwa, wasichana walichukuliwa kama "wake" na askari, huku kuweza kuishi kulitegemea mihogo mikavu chache.

"Naliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoa msaada kwa watoto walioathiriwa na migogoro," mtoto huyo amesema. "Hii itasaidia kuwalinda, kuhakikisha upatikanaji wa elimu na huduma za afya, na kuwaepusha na ukatili."

Virginia Gamba, mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na migogoro ya kivita, ametoa ripoti kuwa, matukio 32,990 dhidi ya watoto 22,557 katika maeneo 26 yalitokea katika sehemu zenye migogoro Mwaka 2023, ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya kila mwaka katika muongo takriban mmoja uliopita. Maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni pamoja na Maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu, DRC, Nigeria, Somalia na Sudan.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha